وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا(1) Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu, |
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا(2) Na kwa wanao toa kwa upole, |
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا(3) Na wanao ogelea, |
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا(4) Wakishindana mbio, |
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا(5) Wakidabiri mambo. |
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ(6) Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka, |
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ(7) Kifuate cha kufuatia. |
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ(8) Siku hiyo nyoyo zitapiga piga, |
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ(9) Macho yatainama chini. |
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ(10) Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? |
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً(11) Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? |
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ(12) Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! |
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ(13) Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, |
فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ(14) Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! |
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ(15) Je! Imekufikia hadithi ya Musa? |
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى(16) Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: |
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ(17) Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. |
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ(18) Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? |
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ(19) Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. |
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ(20) Basi alimwonyesha Ishara kubwa. |
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ(21) Lakini aliikadhibisha na akaasi. |
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ(22) Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. |
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ(23) Akakusanya watu akanadi. |
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ(24) Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. |
فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ(25) Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. |
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ(26) Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. |
أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا(27) Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! |
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا(28) Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. |
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا(29) Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. |
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا(30) Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. |
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا(31) Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, |
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا(32) Na milima akaisimamisha, |
مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ(33) Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. |
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ(34) Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, |
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ(35) Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, |
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ(36) Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, |
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ(37) Basi ama yule aliye zidi ujeuri, |
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا(38) Na akakhiari maisha ya dunia, |
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ(39) Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! |
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ(40) Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, |
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ(41) Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! |
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا(42) Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? |
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا(43) Una nini wewe hata uitaje? |
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا(44) Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. |
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا(45) Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. |
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا(46) Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. |