Surah Maidah aya 32 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ﴾
[ المائدة: 32]
Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Because of that, We decreed upon the Children of Israel that whoever kills a soul unless for a soul or for corruption [done] in the land - it is as if he had slain mankind entirely. And whoever saves one - it is as if he had saved mankind entirely. And our messengers had certainly come to them with clear proofs. Then indeed many of them, [even] after that, throughout the land, were transgressors.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.
Kwa sababu ya uasi huo na kupenda kwa baadhi ya watu kuwafanyia uadui wenginewe, ndio tukawajibisha kumuuwa muuwaji, kwani mwenye kumuuwa mtu bila ya sababu zinazo pasa kisasi, au bila ya kufanya uharibifu katika nchi, ni kama amewauwa watu wote. Yeye huyo amemwaga damu za watu, na amewashajiisha wengine wafanye kama hayo. Kwa hivyo kumuuwa mmoja ni kama kuwauwa watu wote kwa kujiletea maudhiko ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake. Na mwenye kumhuisha mtu kwa kumlipia kisasi, basi ni kama amewahuisha watu wote kwa kuhifadhi damu ya wanaadamu isimwagwe ovyo. Huyo anastahiki thawabu nyingi kutokana na Mola wake Mlezi. Sisi tumewatumia Mitume wetu kutilia mkazo hukumu yetu kwa dalili na hoja. Kisha baadaye wengi miongoni mwa Wana wa Israili walipindukia mipaka katika uharibifu wao katika nchi. Maneno haya yanaonyesha kuwa kumfanyia uadui mtu mmoja ni kuwafanyia jamii ya watu, na kulipa kisasi ndio kuhuisha jamii. Katika Sharia ya Kiislamu kisasi ni haki ya waliy-amri, yaani aliye mkhusu maiti. Akipenda atasamehe achukue fidiya, na akipenda atataka kisasi na akitimize. Naye anapo samehe anayo haki ya kumfedhehesha mkosefu akiwa amekithiri uwovu wake na uharibifu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.
- Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba
- Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na
- Ni kama mfano wa walio kuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja uovu wa mambo yao.
- Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye
- Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira,
- Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya haki. Na wao
- Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo
- Wakaja kwa baba yao usiku wakilia.
- Na Kitabu kilicho andikwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers