Surah Anam aya 152 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴾
[ الأنعام: 152]
Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And do not approach the orphan's property except in a way that is best until he reaches maturity. And give full measure and weight in justice. We do not charge any soul except [with that within] its capacity. And when you testify, be just, even if [it concerns] a near relative. And the covenant of Allah fulfill. This has He instructed you that you may remember.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka.
Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa ya kuyahifadhi na kuyakuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo yatima afike umri wa uwongofu, atapo weza mwenyewe kuendesha mambo yake baraabara. Hapo tena ndio mpeni mali yake. Wala msipunje vipimo na mizani kwa kupunguza mnapo toa, au kuongeza mnapo chukua. Bali pimeni kwa uadilifu kama muwezavyo. Na Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi ila kwa kadiri iwezavyo bila ya karaha. Na mkisema neno katika kuhukumu, au ushahidi, au khabari, au mfano wa hayo, basi msikengeuke mkaacha uadilifu na ukweli. Bali hakikisheni kusema sawa, bila ya kuzingatia makhusiano ya jinsi, yaani uke na ume, au rangi, au ujamaa au ushemeji. Wala msitengue ahadi za Mwenyezi Mungu alizo chukua kwenu kwa taklifu, wala ahadi zilio baina yenu wenyewe kwa wenyewe, katika mambo yaliyo fungamana na maslaha yaliyo ruhusiwa kisharia. Bali timizeni ahadi hizi zote. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa kutilia mkazo mjitenge na yaliyo katazwa, na mkumbuke kuwa Sharia ni kwa ajili ya maslaha yenu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao wanao waomba badala yake hawahukumu chochote. Hakika
- Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na
- Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kati
- Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
- Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi
- Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.
- Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
- Na Mwenyezi Mungu ana majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu,
- Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
- Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



