Surah Baqarah aya 228 , Swahili translation of the meaning Ayah.

  1. Arabic
  2. tafsir
  3. mp3
  4. English
Quran in Swahili QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili - Ali Muhsen Alberwany & English - Sahih International : Surah Baqarah aya 228 in arabic text(The Cow).
  
   

﴿وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
[ البقرة: 228]

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t'ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Surah Al-Baqarah in Swahili

Swahili Translation - Al-Barwani

English - Sahih International


Divorced women remain in waiting for three periods, and it is not lawful for them to conceal what Allah has created in their wombs if they believe in Allah and the Last Day. And their husbands have more right to take them back in this [period] if they want reconciliation. And due to the wives is similar to what is expected of them, according to what is reasonable. But the men have a degree over them [in responsibility and authority]. And Allah is Exalted in Might and Wise.


Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili


Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka tahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.


Yawapasa watalaka wangojee bila ya kufanya pupa ya kuolewa muda wa hedhi tatu , ili kuhakikisha hawana mimba na kujipa nafasi ya kumkinika kurejeana. Wala si halali kwao kuficha mimba au damu ya hedhi. Huo ndio mwendo wa wanawake wanao muamini Mwenyezi Mungu na kukutana naye Siku ya Akhera. Na waume zao wanayo haki kuwarejea katika ule muda wa eda. Na wanaume wanapo tumia haki wakusudie kupatana si kudhuru. Wanawake nao wana haki mfano wa jukumu lilio juu yao katika mambo yasio kuwa kinyume na Sharia Tukufu (2). Na wanaume wana daraja juu yao ya ulinzi na kuyahifadhi maisha ya nyumbani na mambo ya watoto. Mwenyezi Mungu Subhanahu yuko juu ya waja wake, na Yeye ndiye anawatungia sharia zinazo wafikiana na hikima. (1) Zingatia: Khabari ya eda ya mtalaka limefasiriwa neno -Qurui- na wanazuoni wengi kuwa ni -Hedhi-. Na wamefasiri Shafii (na Malik) kuwa ni -tahara-. Khabari nyengine za eda zitakuja baadae. Sharia ya eda imekuja ili kuhakikisha kuwa ipo mimba au hapana, kwani hayo hayawezi kuhakikishwa ila baada ya kupita hedhi (au tahara) tatu, kwani mbegu za uzazi haziwezi kuishi baada ya hedhi tatu. Mwenye mimba kwa kawaida hatoki hedhi, na akitoka ni mara moja au sana mara mbili. Kwani hakika hapo ile mimba huwa imepevuka kwa muda huo hata kufikia kujaza eneo lote la tumbo la uzazi, na kwa hivyo ikazuia kuteremka damu ya mwezi. Hiyo ni kudra ya Mwenyezi Mungu katika kuumba kwake, na hayakuwa hayo yanajuulikana na Waarabu, na wala hayakuwa yajuulikaane na Nabii asiye jua kusoma. Lakini Mwenyezi Mungu alimteremshia Qurani, akamfunza yeye na akaufunza umma wake. Na sababu ya pili ya sharia ya eda ni kumpa fursa ya mtalaka kurejea kwa mumewe baada ya kuwaza na kufikiri na kutua. Na hapo ni mume kusema: -Nimekurejea-. Lakini hii itahisabiwa ni moja katika talaka tatu. Mwenyezi Mungu amempa mwanamke haki kama zile zinazo mwajibikia yeye. Na mwanamume amepewa cheo cha ulinzi na kuhifadhi. Na juu yake ni waajibu wa uadilifu. Uislamu ndio ulio mpa mwanamke haki ambazo hakupata kupewa na mila zote zilizo tangulia. Kwa Warumi mwanamke alikuwa ni kijikazi wa nyumba ya mumewe. Ana jukumu, lakini hana haki. Hali kadhaalika kwa Waajemi. (Na vivyo hivyo katika dini za Kiyahudi, Kikristo na Kibaniani.) Paulo ameandika katika 1 Korintho: -Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Na wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu kunena katika kanisa.- - 1 Korinth. 14.34-35. -Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.- 1 Korinth. 11.7.9 -Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa..- 1 Timotheo 2.11-14. Na hapana popote katika Biblia panapo kataza Mayahudi au Wakristo kuoa wake wengi, isipo kuwa kauli moja tu ya Paulo inayo mpendekeza Askofu aoe mke asiye zidi mmoja. Kauli hiyo iko katika Waraka wa Kwanza wa Paulo kwa Timotheo 3.2: -Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, n.k.- Je, ni Uislamu au Ukristo ulio mweka chini mwanamke?)

English Türkçe Indonesia
Русский Français فارسی
تفسير Bengali Urdu

listen to Verse 228 from Baqarah


Ayats from Quran in Swahili


Quran Surah in Swahili :

Al-Baqarah Al-'Imran An-Nisa'
Al-Ma'idah Yusuf Ibrahim
Al-Hijr Al-Kahf Maryam
Al-Hajj Al-Qasas Al-'Ankabut
As-Sajdah Ya Sin Ad-Dukhan
Al-Fath Al-Hujurat Qaf
An-Najm Ar-Rahman Al-Waqi'ah
Al-Hashr Al-Mulk Al-Haqqah
Al-Inshiqaq Al-A'la Al-Ghashiyah

Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :

Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Surah Baqarah Ahmed El Agamy
Ahmed Al Ajmy
Surah Baqarah Bandar Balila
Bandar Balila
Surah Baqarah Khalid Al Jalil
Khalid Al Jalil
Surah Baqarah Saad Al Ghamdi
Saad Al Ghamdi
Surah Baqarah Saud Al Shuraim
Saud Al Shuraim
Surah Baqarah Abdul Basit Abdul Samad
Abdul Basit
Surah Baqarah Abdul Rashid Sufi
Abdul Rashid Sufi
Surah Baqarah Abdullah Basfar
Abdullah Basfar
Surah Baqarah Abdullah Awwad Al Juhani
Abdullah Al Juhani
Surah Baqarah Fares Abbad
Fares Abbad
Surah Baqarah Maher Al Muaiqly
Maher Al Muaiqly
Surah Baqarah Muhammad Siddiq Al Minshawi
Al Minshawi
Surah Baqarah Al Hosary
Al Hosary
Surah Baqarah Al-afasi
Mishari Al-afasi
Surah Baqarah Yasser Al Dosari
Yasser Al Dosari


Sunday, December 22, 2024

Please remember us in your sincere prayers