Surah Baqarah aya 229 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴾
[ البقرة: 229]
T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Divorce is twice. Then, either keep [her] in an acceptable manner or release [her] with good treatment. And it is not lawful for you to take anything of what you have given them unless both fear that they will not be able to keep [within] the limits of Allah. But if you fear that they will not keep [within] the limits of Allah, then there is no blame upon either of them concerning that by which she ransoms herself. These are the limits of Allah, so do not transgress them. And whoever transgresses the limits of Allah - it is those who are the wrongdoers.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu.
talaka ni mara mbili. Baada ya kila talaka ana haki mume kukaa naye kwa kumrejea kabla ya kwisha siku za eda, au kumrejesha katika dhamana yake kwa kumwoa upya. Na katika hali hiyo inapasa makusudio yake ni kukaa naye kwa uadilifu na kumtendea wema, au kuachana kwa ihsani na heshima bila ya kukhasimiana. Wala si halali kwenu, enyi waume, kuchukua chochote mlicho wapa wanawake ila mkikhofu kuwa hamtoweza kufuata haki za uke na ume alizo kubainishieni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, na akaku lazimisheni mzifuate. Mkikhofu, enyi Waislamu, kutofuata haki za mume na mke vilivyo kama alivyo eleza Mwenyezi Mungu basi ameamrisha mke atoe mali kwa ajili ya kutokana na mumewe. Na hizi ni hukumu zilizo pitishwa, msiende kinyume nazo, mkazipindukia. Mwenye kufanya hivyo amejidhulumu nafsi yake na amedhulumu jamii anayo ishi kati yake. Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ameifanyia sharia talaka, na akampa mwanamume kwanza uwezo wa kuacha. Baadhi ya watu wanadhani kuwa haya huleta madhara katika maisha na kusahilisha kuvunjika nyumba za watu. (a) Ama kupewa haki ya kuacha mwanamume kwa hakika hakupewa haki hiyo bila ya masharti yoyote. Katika masharti hayo aliyo wekewa ni: KWANZA hana ruhusa kuacha ila talaka moja ya kuweza kurejea, yaani anakuwa na haki ya kumrejea mke kabla ya kwisha eda. Ama amrejee naye yu ndani ya eda au amwache, na hivyo tena ni dalili ya hadi ya kuchukiana, na hapana maisha ya mume na mke tena kuchukiana kumefika hadi hiyo. PILI asimwache wakati wa hedhi, kwani wakati huo mwanamke huwa na hamaki, kwa hivyo huwa hapana utulivu. Na huenda hiyo hedhi ndiyo sababu ya hizo chuki zilizo zidi. Basi asiache mpaka mambo yawe yametua. TATU asimwache naye yumo katika tahara aliyo kwisha muingilia, kwani hiyo yaweza kuonekana huko kuchukiana kunatokana na kutokuwa na raghba na mkewe. Basi mambo yakiwa hivi talaka inakuwa katika hali ya chuki iliyo na nguvu, na kukatika mapenzi ya daima.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akasema: Ama aliye dhulumu basi tutamuadhibu, na kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi amuadhibu adhabu
- Mna nini hata hamsemi?
- Hayo ni kwa sababu walikuwa wanawajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini wakawakataa, ndipo
- Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji
- Na unapo soma Qur'ani tunaweka baina yako na wale wasio iamini Akhera pazia linalo wafunika.
- Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?
- Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao.
- Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.
- Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
- Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers