Surah Baqarah aya 266 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ﴾
[ البقرة: 266]
Je! Yupo mmoja wenu anaye penda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu ipitayo mito kati yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia naye hali ana watoto wanyonge, kikapigwa na kimbunga chenye moto, kikaungua? Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Ishara ili mpate kufikiri.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Would one of you like to have a garden of palm trees and grapevines underneath which rivers flow in which he has from every fruit? But he is afflicted with old age and has weak offspring, and it is hit by a whirlwind containing fire and is burned. Thus does Allah make clear to you [His] verses that you might give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Yupo mmoja wenu anaye penda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu ipitayo mito kati yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia naye hali ana watoto wanyonge, kikapigwa na kimbunga chenye moto, kikaungua? Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Ishara ili mpate kufikiri.
Hapana yeyote katika nyinyi anaye penda kuwa na kitalu cha mitende na mizabibu na mito inapita kati yake na kimezaa kila namna ya matunda ayatakayo, naye hali amekwisha kuwa mkongwe na akawa na watoto wadogo wanyonge hawawezi kazi wala yeye hajiwezi kwa ukongwe wake, kikaja kitalu chake kikakauka kwa upepo mkali wenye moto, na miti ikaungua, wakati ambao yeye mwenyewe na watoto ndio wamo katika shida ya kuhitaji. Basi hali kadhaalika shani ya mwenye kutoa sadaka na akafuatishia masimbulizi na maudhi na riya, kujionyesha kwa watu, ambayo hayo yakapoteza thawabu zote za sadaka zake, na wala hawezi tena kutoa sadaka kwa kujitengezea nafsi yake. Kwa bayana kama hizi ndio Mwenyezi Mungu anakuonyesheni Ishara ili mpate kutafakari na kujifunza. Ilimu ya kisasa inaeleza kuwa katika anga pepo kali hugongana zikatoka radi na umeme na mvua. Huenda ukatokea moto kwa umeme kwa kugongana mawingu, au pengine huweza kutokea vimondo kutokana na volkano (burkani) iliyo karibu ikateketeza miti na chochote kilicho katika sehemu hizo. Qurani inaashiria maana zote hizo.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
- Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu -
- Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni
- Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na
- Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
- Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
- Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake,
- Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
- Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi
- Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



