Surah Baqarah aya 265 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴾
[ البقرة: 265]
Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And the example of those who spend their wealth seeking means to the approval of Allah and assuring [reward for] themselves is like a garden on high ground which is hit by a downpour - so it yields its fruits in double. And [even] if it is not hit by a downpour, then a drizzle [is sufficient]. And Allah, of what you do, is Seeing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
Hali ya wanao toa mali zao kwa kutaka kumridhi Mwenyezi Mungu na kuzithibitisha nafsi zao juu ya Imani, ni kama hali ya bustani, au kitalu, kwenye ardhi yenye rutuba iliyo nyanyuka (1) inayo faidika kwa maji mengi au kidogo. Ikija mvua kubwa huzaa mazao yake mardufu; na ikitopata mvua kubwa basi hata manyunyu kidogo hutosha kwa vile ardhi ni nzuri yenye kutoa mazao katika hali zote mbili. Basi Waumini wenye nyoyo safi hazipotei amali zao. Na vitendo vyenu havifichiki kwa Mwenyezi Mungu. (1) Neno la Qurani -ardhi iliyo nyanyuka- linaashiria yaliyo vumbuliwa na ilimu za sayansi za kisasa, kuwa maji ya chini yanakuwa yako mbali na mizizi. Kwa hivyo mizizi haiozi na vijizizi vidogo vinapata kunyonya chakula kwa wasaa na pia kuvuta pumzi. Kwa hivyo mazao yanakuwa mema, kwa mvua ijayo au hata manyunyu. (Nasi twajua mikarafuu au minazi ya bondeni haina maisha wala haistawi.)
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee
- Isipo kuwa watu wa kuliani.
- Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
- Na walio amini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawatia miongoni mwa watu wema.
- Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi
- Na mwezi utapo patwa,
- Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.
- Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
- Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



