Surah Baqarah aya 282 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ ۗ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾
[ البقرة: 282]
Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, when you contract a debt for a specified term, write it down. And let a scribe write [it] between you in justice. Let no scribe refuse to write as Allah has taught him. So let him write and let the one who has the obligation dictate. And let him fear Allah, his Lord, and not leave anything out of it. But if the one who has the obligation is of limited understanding or weak or unable to dictate himself, then let his guardian dictate in justice. And bring to witness two witnesses from among your men. And if there are not two men [available], then a man and two women from those whom you accept as witnesses - so that if one of the women errs, then the other can remind her. And let not the witnesses refuse when they are called upon. And do not be [too] weary to write it, whether it is small or large, for its [specified] term. That is more just in the sight of Allah and stronger as evidence and more likely to prevent doubt between you, except when it is an immediate transaction which you conduct among yourselves. For [then] there is no blame upon you if you do not write it. And take witnesses when you conclude a contract. Let no scribe be harmed or any witness. For if you do so, indeed, it is [grave] disobedience in you. And fear Allah. And Allah teaches you. And Allah is Knowing of all things.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Enyi mlio amini! Mkikopeshana deni kwa muda, inatakikana huo muda ujuulikane. Nanyi muandikiane ili kuhifadhi haki na usitokee mzozo. Na lazima mwenye kuandika awe mtu muadilifu katika uandishi wake. Wala muandishi asikatae kuandika, kwani hivyo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya ilimu aliyo mfunza naye alikuwa haijui. Basi aandike lile deni kwa mujibu anavyo kubali yule mwenye kukopa. Naye huyo mwenye kukopa amwogope Mola wake Mlezi, asipunguze hata chembe katika deni lilio juu yake. Pindi akiwa mwenye kukopa hawezi kujiendesha, wala hayawezi mambo vilivyo, au ni mnyonge kwa udogo au ugonjwa au ukongwe, au akawa hawezi kuandikisha kwa ajili ya ububu au uzito wa ulimi au kutojua lugha inayo andikiwa huo waraka, basi mlinzi wake wa kisharia au hakimu au aliye mkhiari yeye, awe ndiye naibu wake wa kutoa imla ya kuliandika hilo deni kwa uadilifu ulio timia. Na washuhudisheni deni hilo wanaume wawili miongoni mwenu. Ikiwa hawakupatikana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili, washuhudie ili pindi mtu akirusha waweze kutoa ushahidi wao, na akisahau mmoja mwengine aweze kumkumbusha. Wala haijuzu kujizuia kutoa ushahidi pindi unapo takikana. Wala msipuuze kuandika kidogo na kikubwa maadamu ni deni la kulipwa baadae. Hivyo ndio uadilifu wa sharia ya Mwenyezi Mungu, na ndio kuwa na nguvu zaidi kuwa ni dalili ya ukweli wa ushahidi, na ndio vyema zaidi kuondoa shaka shaka baina yenu. Ila ikiwa jambo lenyewe ni biashara ya mkono-kwa-mkono mnayo uzuiana baina yenu, hapo si lazima kuandikiana, kwani hapana dharura ya hayo. Na inatakikana lakini katika kuuziana pawepo mashahidi ili kuepusha ugomvi. Na tahadharini asipate madhara yoyote mwenye kuandika au mwenye kushuhudia. Hayo itakuwa ni kutokana na utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na mkhofuni Mwenyezi Mungu, na ogopeni heba yake katika anayo amrisha na anayo yakataza. Hivyo ndio nyoyo zenu zitalazimika kufuata insafu na uadilifu. Na Mwenyezi Mungu anakubainishieni haki zenu na waajibu ulio juu yenu. Naye ni Mjuzi wa kila kitu - vitendo vyenu na vinginevyo. Aya hii inahakikisha misingi ya kuthibitisha. Inahakikisha msingi wa kuandikiana. Hukumu haiwi kwa chini kuliko mashahidi wawili walio wanaume waadilifu, au mwanamume mmoja na wanawake wawili. Na imelazimika mwandishi awe muadilifu, na wawepo mashahidi panapo kuwapo mafungamano. Lakini hapana lazima ya mashahidi ikiwa muamala wenyewe wa papo kwa papo, nipe nikupe, mkono kwa mkono. Pia aya inahakikisha kuwa mtu aliye pumbaa, au hawezi kujiendeshea mambo yake mtu mwenyewe, au mnyonge dhaifu, basi lazima awe na mtu kuwa ni wakili wake wa kumtendea badala yake. Na pindi ikiwa ni safarini na hapana mtu wa kuandika, basi yatosha kutoa kitu kiwe rahani akamate mwenye kukopesha
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku
- Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
- Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
- Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao ndio
- Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
- Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini;
- Unao babua ngozi ya kichwa!
- Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu
- Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na
- Na ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi yenye
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers