Surah Maidah aya 48 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴾
[ المائدة: 48]
Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We have revealed to you, [O Muhammad], the Book in truth, confirming that which preceded it of the Scripture and as a criterion over it. So judge between them by what Allah has revealed and do not follow their inclinations away from what has come to you of the truth. To each of you We prescribed a law and a method. Had Allah willed, He would have made you one nation [united in religion], but [He intended] to test you in what He has given you; so race to [all that is] good. To Allah is your return all together, and He will [then] inform you concerning that over which you used to differ.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Na wewe, ewe Nabii, tumekuteremshia Kitabu kikamilifu, nacho ni Qurani, chenye kushikamana na haki katika hukumu zake zote na khabari zake, chenye kuwafikiana na kuthibitisha Vitabu vyetu vilivyo tangulia, na kinavishuhudia kuwa ni Vitabu vya Mwenyezi Mungu, na kinalinda yaliyo sahihi, kwa sababu hii Qurani haibadiliki. Basi hukumu baina ya Watu wa Kitabu, Mayahudi na Wakristo, wakikutaka uwahukumu kwa mujibu alivyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Wala katika hukumu yako usifuate matamanio yao na matakwa yao, usije ukapotoka ukaacha Haki iliyo kujia. Kila umma katika nyinyi watu, tumeujaalia kuwa na njia yake ya kuitambua Haki, na njia iliyo wazi ya Dini ya kuifuata. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka angeli kufanyeni nyote kundi moja lililo wafikiana, lenye mwendo mmoja, hazikhitalifiani njia zake za kupita kwa zama zote. Lakini Yeye amekujaalieni hivi ili iwe kama mtihani kwenu katika hizo Sharia alizo kupeni, atambulikane mwenye kutii na mwenye kuasi. Basi tumieni fursa hii, na mfanye haraka kuwania kutenda vitendo vya kheri. Kwani marejeo yenu nyote yatakuwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Hapo atakwambieni hakika ya hayo mliyo kuwa mkikhitalifiana, na kila mmoja wenu atalipwa kwa amali yake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wale walio kadhibisha Ishara zetu, tutawapururia pole pole kwa namna ambayo wenyewe hawaijui.
- Basi khofu ilipo mwondoka Ibrahim, na ikawa ile bishara imemfikia, alianza kujadiliana nasi juu ya
- Na kwa usiku unapo tanda!
- Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyo fanya naye.
- Yeye ndiye Mwenye kujua yanayo onekana na yasio onekana; Mkuu Aliye tukuka.
- Hakika hao mnao waomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Hebu waombeni,
- Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio walio
- Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni.
- Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu
- Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers