Surah Maidah aya 49 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ﴾
[ المائدة: 49]
Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And judge, [O Muhammad], between them by what Allah has revealed and do not follow their inclinations and beware of them, lest they tempt you away from some of what Allah has revealed to you. And if they turn away - then know that Allah only intends to afflict them with some of their [own] sins. And indeed, many among the people are defiantly disobedient.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.
Na wewe ewe Mtume! Tumekuamrisha uhukumu baina ya watu kwa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matakwa yao katika kuhukumu. Na wahadharishe wasije kukugeuza ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Pindi wakiipuuza hukumu ya Mwenyezi Mungu na wakataka nyengineyo, basi jua kuwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapatiliza kwa kuwafisidia mambo yao, kwa vile zilivyo kwisha fisidika nafsi zao kwa sababu ya madhambi yao waliyo yatenda kwa kukhalifu hukumu zake na Sharia yake. Kisha atawalipa vitendo vyao vyote huko Akhera. Na hakika watu wengi ni wenye kuziasi hukumu za Sharia. Maneno haya yanatukuza Sharia ya Kiislamu katika kuwahukumu watu. Kwanza inatukuka kwa kuwa ni hukumu ya uadilifu na haifuati mipango ya watu ijapo kuwa ni mipotovu, bali inahukumu juu ya hiyo mipango ya watu kwa kheri na shari. Pili Kanuni huwa katika dola ni moja tu kwa watu wote na matabaka yote.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.
- Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
- Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.
- Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,
- Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi?
- Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa
- Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
- Wale wanao wabeuwa Waumini wanao toa sadaka nyingi na wasio nacho cha kutoa ila kadri
- Ngoja tu, na wao wangoje pia.
- Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers