Surah An Nur aya 58 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِيَسْتَأْذِنكُمُ الَّذِينَ مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ وَالَّذِينَ لَمْ يَبْلُغُوا الْحُلُمَ مِنكُمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ ۚ مِّن قَبْلِ صَلَاةِ الْفَجْرِ وَحِينَ تَضَعُونَ ثِيَابَكُم مِّنَ الظَّهِيرَةِ وَمِن بَعْدِ صَلَاةِ الْعِشَاءِ ۚ ثَلَاثُ عَوْرَاتٍ لَّكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ وَلَا عَلَيْهِمْ جُنَاحٌ بَعْدَهُنَّ ۚ طَوَّافُونَ عَلَيْكُم بَعْضُكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴾
[ النور: 58]
Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.
Surah An-Nur in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, let those whom your right hands possess and those who have not [yet] reached puberty among you ask permission of you [before entering] at three times: before the dawn prayer and when you put aside your clothing [for rest] at noon and after the night prayer. [These are] three times of privacy for you. There is no blame upon you nor upon them beyond these [periods], for they continually circulate among you - some of you, among others. Thus does Allah make clear to you the verses; and Allah is Knowing and Wise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.
Enyi mlio amini! Yakupaseni muamrishe watumishi wenu na vijana wenu ambao bado hawajabalighi wasikuingilieni vyumbani mwenu ila baada ya kutaka idhini katika nyakati tatu, nazo ni kabla ya Swala ya alfajiri, na pale mnapo punguza nguo zenu wakati wa kupumzika mchana, na baada ya Swala ya Isha mnapo jitayarisha kulala. Kwani nyakati hizi mtu hubadilisha mavazi ya kulalia badala ya mavazi ya kutokea, na huonekana sehemu za mwili ambazo hazifai kuonekana. Wala hapana ubaya kwenu wala kwao kuingia bila ya ruhusa nyakati nyenginezo, kwa sababu ni jamba la ada watu wa nyumbani kupitiana kwa maslaha yao. Na kwa uwazi wa namna hii Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya za Qurani ili akuwekeeni wazi hukumu. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mkunjufu wa ujuzi, Mkubwa wa hikima, anajua yanayo silihi kwa waja wake, na anawatungia Sharia zinazo wanasibu, na kwa kadri ya haja yao. -Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamikiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Swala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Swala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.- Aya hii tukufu ni moja katika Aya zinazo elekeza nadhari ya watu wazingatie yaliyo laiki katika jamii za watu khasa ndani ya ukoo. Nayo kuwa kuchanganyika kwa watumishi na watoto katika aila yao huenda kukapindukia mipaka ya hishima za maingiano, wakawa wanawaingilia wenginewe bila ya kutaka idhini katika nyakati maalumu zilizo tajwa katika Aya. Na kwa kuwa nyakati hizo ni nyakati za faragha na uhuru wa binafsi, na kuvua nguo nzito nzito, Aya hii imekusudia kuweka Sharia ya kutaka idhini katika nyakati hizo kutokana na watumishi na vijana ili wasione ambayo yanahisabiwa kuwa ni siri, ambayo ni kama utupu ambao wapasa kusitiriwa. Na kwa hivyo wanaelekezwa watu wa ukoo wavae mavazi yanayo kuwa laiki ya kukabiliana hata wao kwa wao, ili hishima yao ibaki imehifadhika, na uhuru wao umedhaminika, na adabu zao zimechungika. Na Qurani ndio inaayo faa khasa kutuongoza tufuate mwendo ulio bora na wa juu. (Ikiwa watoto wa nyumbani haiwafalii kuwaingilia watu katika nyakati hizo za faragha zilizo tajwa, seuze watu mbali!)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
- Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa.
- Hakika wao wanaiona iko mbali,
- Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa
- Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu.
- Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa
- Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la
- Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote
- Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
- Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah An Nur with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah An Nur mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Nur Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers