Surah Qasas aya 77 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ﴾
[ القصص: 77]
Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.
Surah Al-Qasas in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But seek, through that which Allah has given you, the home of the Hereafter; and [yet], do not forget your share of the world. And do good as Allah has done good to you. And desire not corruption in the land. Indeed, Allah does not like corrupters."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.
Na katika utajiri na neema alizo kupa Mwenyezi Mungu toa fungu kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, na tenda amali kwa ajili ya makaazi ya Akhera. Na wala usiinyime nafsi yako fungu lake kwa matumizi ya halali katika dunia. Na wafanyie wema waja wa Mwenyezi Mungu, kama vile alivyo kufanyia wema wewe kwa neema zake. Wala usifanye uharibifu katika ardhi ukapita mipaka ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu hawafurahii mafisadi kwa vitendo vyao viovu. Basi Qaruni hakusikia nasaha ya watu wake, na akasahau fadhila ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yake. Na akajifanya hajui kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza wengi walio mzidi yeye sana katika uwezo na mazoezi ya kuchuma mali kwa njia mbali mbali za uchumi. Na wakosefu hawaulizwi madhambi yao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua. Basi wataingizwa Motoni bila ya hisabu. Kuulizwa kwao ni kwa ajili ya kutahayarishwa tu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha
- (Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.
- Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua
- Ni Nyota yenye mwanga mkali.
- Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye
- Hakika Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni ambapo wingi wenu ulikupandisheni
- Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri.
- Na siku itapo simama Saa, siku hiyo watagawanyika.
- Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
- Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Qasas with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Qasas mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Qasas Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers