Surah Fatir aya 13 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ﴾
[ فاطر: 13]
Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.
Surah Fatir in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
He causes the night to enter the day, and He causes the day to enter the night and has subjected the sun and the moon - each running [its course] for a specified term. That is Allah, your Lord; to Him belongs sovereignty. And those whom you invoke other than Him do not possess [as much as] the membrane of a date seed.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.
Yeye huuingiza usiku katika mchana, na mchana katika usiku. Matokeo yake ni kuwa saa zao hurefuka na hufupika kwa mujibu wa mipango ya hikima miaka nenda miaka rudi. Na Yeye amelifanya jua na mwezi kutumika kwa manufaa yenu. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu utao ishia kwake. Huyo mwenye shani kuu ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye kuyapanga mambo yenu. Ufalme ni wake Yeye peke yake. Na hao wengineo mnao waomba kuwa ni miungu mnao waabudu hawawezi kumiliki hata ugozi mwembamba ule wa kokwa ya tende. Basi inakuwaje wastahili kuabudiwa? Aya hii tukufu inaonyesha kuwa jua lina muda utakao kwisha baadae. Na huenda kuwa huo ndio utao kuwa Mwisho kwa mujibu wasemavyo wataalamu wa ilimu ya Falaki (Astronomy) kwamba jua linaunguza kuni zake za Dharra (Nuclear fuel) nayo ni Hydrogen inayo geuka kuwa Helium. Huenda kuwa ukisha muda wa jua ndio Msiba Mkuu wa Ulimwengu wote.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
- Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na
- Hakika mtu ameumbwa na papara.
- Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.
- Na wajumbe wetu walipo mjia Ibrahim na bishara, walisema: Hakika sisi hapana shaka tutawahiliki watu
- Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa
- Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
- Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
- Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili ibainike njia ya wakosefu.
- Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Fatir with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Fatir mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Fatir Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers