Surah Nisa aya 131 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدًا﴾
[ النساء: 131]
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And to Allah belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. And We have instructed those who were given the Scripture before you and yourselves to fear Allah. But if you disbelieve - then to Allah belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. And ever is Allah Free of need and Praiseworthy.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa.
Kiini cha Dini ni kumnyenyekea Mwenye kuumba ulimwengu, Mwenye utukufu na ukarimu, na kuukubali ufalme wake usio na ukomo. Kwani ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Na kwa huu Ufalme usio na ukomo amesema: Tumewausia watu wa dini zilizo toka mbinguni, katika Watu wa Kitabu na nyinyi Waislamu, mumkhofu Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na msiwe mnakufuru katika ibada yake, maana Yeye ndiye Mwenye utawala mkubwa kushinda wote. Hapana kitu kilicho toka nje ya utawala wake. Yeye ni Mkwasi, yaani mwenye kujitosha wala hakuhitajiini nyinyi. Juu ya hivyo Yeye anakuhimidini kwa imani yenu, kwani kwa kuwa Yeye ni Mwenye kujitosheleza mwenyewe, juu ya hivyo anasifu na kushukuru vitendo vyema vya waja wake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanakuuliza khabari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga.
- Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na
- (Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema yako.
- Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
- Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba
- Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
- Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele.
- Na matunda mengi,
- Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.
- Kwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers