Surah Ahqaf aya 15 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴾
[ الأحقاف: 15]
Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
Surah Al-Ahqaaf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We have enjoined upon man, to his parents, good treatment. His mother carried him with hardship and gave birth to him with hardship, and his gestation and weaning [period] is thirty months. [He grows] until, when he reaches maturity and reaches [the age of] forty years, he says, "My Lord, enable me to be grateful for Your favor which You have bestowed upon me and upon my parents and to work righteousness of which You will approve and make righteous for me my offspring. Indeed, I have repented to You, and indeed, I am of the Muslims."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
Na tumemuusia mwanaadamu kwa wazazi wake awafanyie wema mkubwa. Kwani mama yake amechukua mimba yake kwa mashaka, na akamzaa kwa mashaka. Na muda wa kuchukuliwa mimba mpaka kuachishwa ziwa ni miezi thalathini. Muda wote huo mama kapitikiwa na kila namna ya machungu. Mpaka huyo mtu alipo fikilia ukamilifu wa nguvu zake na akili yake, na akafikia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Nijaalie niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nijaalie nitende vitendo vyema utavyo viridhi Wewe, na ujaalie huo wema wapate pia dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako kwa kila dhambi, na mimi ni miongoni wa Waislamu, yaani walio zisalimisha nafsi zao kwako. Uchache wa mimba ni miezi sita, kwa kauli yake Mtukufu: - Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini.- Na kauli yake Mtukufu: -Na kumwachisha ziwa kwake ni miaka miwili-, na kauli yake Mtukufu: -Na wazazi wa kike huwanyonyesha wana wao miaka miwili kaamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha.- Basi ukitoa muda wa kuachisha ziwa kutokana na muda wa mimba na kunyonyesha inabakia muda wa mimba ni miezi sita. Na haya yanawafikiana na iliyo thibiti kwa ilimu za sayansi kwamba mtoto mchanga akizaliwa baada ya mimba ya miezi 6 anaweza kuishi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.
- Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu ulio kwisha pita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo
- Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu.
- Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao,
- Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi!
- Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka,
- Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?
- Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake,
- Je wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na hukumu
- Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Ahqaf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Ahqaf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Ahqaf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers