Surah Baqarah aya 150 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴾
[ البقرة: 150]
Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And from wherever you go out [for prayer], turn your face toward al-Masjid al-Haram. And wherever you [believers] may be, turn your faces toward it in order that the people will not have any argument against you, except for those of them who commit wrong; so fear them not but fear Me. And [it is] so I may complete My favor upon you and that you may be guided.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.
Jilazimishe kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu katika mambo ya kuelekea Kibla, na kuwa na pupa nayo wewe na umma wako. Na uelekeze uso wako uelekee upande wa Msikiti Mtakatifu popote wendapo katika safari zako. Na elekeeni huko popote mtapo kuwapo pande zote za dunia, mkiwa mko safarini au mpo mjini, ili ukatike ule ushindani wa hoja za hao walio khalifu na wanao jadiliana nanyi ikiwa hamkufuata amri hii ya kugeuza Kibla. Mayahudi watasema: Vipi Muhammad anapo sali anaelekea Beitul Muqaddas, na Nabii alielezwa katika vitabu vyetu ni kuwa moja katika sifa zake anaelekea Alkaaba? Na washirikina wa Kiarabu watasema: Vipi anadai kuwa mila yake ni mila ya Ibrahim, naye hafuati Kibla chake? Juu ya vyote hakika hao walio dhulumu walio potoka wakaiacha Haki kutoka pande zote mbili hawatoacha majadiliano yao na upotovu wao, bali watasema: Hakugeuka kuelekea Alkaaba ila kuwa anafuata ile ile dini ya kishirikina ya kaumu yake, na kuupenda ule mji wake. Basi nyinyi msiwabali hao, kwani uchochezi wao hauto kudhuruni. Nanyi niogopeni Mimi, msiikhalifu amri yangu. Kwa amri hii tumetaka kuitimiza neema juu yenu, na Kibla hichi tulicho kuelekezeni ndicho kipelekee kuthibiti kwenu katika uwongofu na kupata tawfiki.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
- Na waonye siku ya majuto itapo katwa amri. Nao wamo katika ghafla, wala hawaamini.
- Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
- Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
- Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
- Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
- Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na
- Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
- Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
- Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake! Hakika amesalitika kwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers