Surah Zumar aya 21 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَلَكَهُ يَنَابِيعَ فِي الْأَرْضِ ثُمَّ يُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَجْعَلُهُ حُطَامًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ﴾
[ الزمر: 21]
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.
Surah Az-Zumar in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Do you not see that Allah sends down rain from the sky and makes it flow as springs [and rivers] in the earth; then He produces thereby crops of varying colors; then they dry and you see them turned yellow; then He makes them [scattered] debris. Indeed in that is a reminder for those of understanding.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.
Ewe usemezwaye! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, akayapitisha kwenye mito na chemchem za katika ardhi, kisha kwa maji hayo akaotesha mimea ya namna mbali mbali. Kisha baada ya kustawi kwake hiyo mimea, ikayabisika ukaiona imekuwa rangi ya manjano baada ya kustawi kwake. Kisha akaifanya imevurugika na kukatika vipande vipande. Hakika kutoka kwenye hali moja na kuingia hali nyengine ni mazingatio kwa wenye akili zilizo nawirika. Huku kuzunguka maji katika maumbile kutoka mbinguni na kufika kwenye ardhi na huko yakenda chini na kutimbuka katika chemchem, hakukuwa kunajuulikana kabla ya katikati za karne ya nane tangu kuzaliwa Nabii Isa a.s. Fikra iliyo zagaa kabla ya hapo ni kuwa maji ya chemchem na mito yanatimbuka kutoka chini ya ardhi kutoka kwenye mashimo na visima katika vina vya bahari.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na msip o mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini.
- Ngoja tu, na wao wangoje pia.
- Ambaye amefundisha kwa kalamu.
- Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu
- Na atakaye mjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya
- Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili
- Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu.
- Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkisha geuka kwenda zenu.
- Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
- Sema: Hakika mimi ninaogopa adhabu ya Siku Kubwa nikimuasi Mola wangu Mlezi.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Zumar with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Zumar mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Zumar Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



