Surah Baqarah aya 22 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾
[ البقرة: 22]
(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[He] who made for you the earth a bed [spread out] and the sky a ceiling and sent down from the sky, rain and brought forth thereby fruits as provision for you. So do not attribute to Allah equals while you know [that there is nothing similar to Him].
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.
Ni Yeye Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye itandika ardhi kwa kudra yake, na akaikunjua ili isahilike kwenu kuweza kuikalia na kunafiika kwayo. Akajaalia juu yenu mbingu zilio nyanyuka na sayari zake mfano wa jengo lililo jengwa vilivyo, na akakuleteeni njia za uhai na neema - nayo ni maji - aliyo yateremsha kutoka mbinguni, akayafanya ndiyo sababu ya kutoa mimea na miti ya matunda ambayo amekuruzukuni faida yake. Basi haifai baada ya haya mkawaza kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika mkawaabudu kama kumuabudu Yeye, kwani Yeye hana mfano wake wala mshirika. Na nyinyi kwa maumbile yenu mnajua kwa yakini kuwa Yeye hana mfano wala mshirika. Basi msiyaharibu maumbile haya. Katika Aya hii ipo sehemu ya kuonesha muujiza wa Qurani Tukufu: nayo ni kauli yake Mtukufu -mbingu kama paa-. Haya asingeyajua Nabii asiyejua kusoma ila kwa ufunuo wa Mwenyezi Mungu, nayo ni kuwa mbingu kwa kisayansi ni kila kilicho izunguka dunia pande zote, na kwa ukomo wowote, na kwa sura yoyote katika anga, mpaka huko juu kabisa kwenye sayari nyenginezo, zilizoenea zisio na mwisho. Zote hizo zinazunguka kwa mpango wa ajabu, na sisi tunapata uvukuto na mngao wake, nazo zinakwenda kwa nguvu ya mvutano kama smaku. Katika sehemu ya mwanzo ya mbingu iliyo tuzunguka lipo anga linalo tukinga kama paa na mianga inayo dhuru kutokana na hizo sayari. Na tabaka hizo huachilia mianga yenye faida tu, ndipo penye mawingu yaletayo mvua.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni ng'ombe gani? Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba
- Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
- Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni.
- Unababua ngozi iwe nyeusi.
- Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye
- Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno
- Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.
- Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu
- Wakasema: Sisi tutamrairai baba yake; na bila ya shaka tutafanya hayo.
- Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers