Surah Kahf aya 28 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا﴾
[ الكهف: 28]
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimt'ii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka.
Surah Al-Kahf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And keep yourself patient [by being] with those who call upon their Lord in the morning and the evening, seeking His countenance. And let not your eyes pass beyond them, desiring adornments of the worldly life, and do not obey one whose heart We have made heedless of Our remembrance and who follows his desire and whose affair is ever [in] neglect.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimtii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka.
Ewe Mtume! Shikamana na usuhuba wa masahaba wako Waumini, wanao muabudu Mwenyezi Mungu peke yake asubuhi na jioni daima, huku wanataka radhi zake. Wala jicho lako lisiwawache hao kuwaangalia wapinzani wa kikafiri kwa kutaka kustarehe nao katika mapambo ya maisha ya dunia. Wala usikubali kuwafukuza Waumini mafakiri katika baraza yako kwa kumridhisha huyo tuliye mghafilisha moyo wake na kutukumbuka Sisi, kwa kuwa yeye mwenyewe hakuwa tayari kwa hayo, na akawa ni mtumwa wa pumbao lake, na mambo yake katika vitendo vyake vyote hayakufuata njia iliyo sawa. Na anapo katazwa Nabii, basi ndio wanakatazwa wengineo (yaani sote sisi). Na hakika Nabii s.a.w. hataki maisha ya dunia na pumbao lake. Lakini makatazo hayo anaelekezewa Nabii ili wenginewe watahadhari na kutaka pumbao la dunia. Kwani ikiwa yaweza kuwa kwake kutaka pumbao la kimwili, basi kila mwanaadamu yaweza kuwa katika nafsi yake. Kwa hivyo ajilinde.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
- Kwa sababu alimjia kipofu!
- Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio
- Na zinazo farikisha zikatawanya!
- Watapata watakacho taka kwa Mola wao Mlezi. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema.
- Yatima aliye jamaa,
- Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.
- Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.
- Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.
- Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Kahf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Kahf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Kahf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers