Surah Araf aya 145 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ﴾
[ الأعراف: 145]
Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We wrote for him on the tablets [something] of all things - instruction and explanation for all things, [saying], "Take them with determination and order your people to take the best of it. I will show you the home of the defiantly disobedient."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu.
Na tulimbainishia Musa katika zile mbao za Taurati kila kitu kilicho khusu mawaidha na hukumu zilizo elezwa mbali mbali, wanazo hitajia watu duniani na Akhera. Na tukamwambia: Zishike hizi mbao baraabara na kwa kuazimia. Na waamrishe watu wako washike yaliyo bora humo, kama kusamehe badala ya kulipiza kisasi, na kuachilia badala ya kungojea, na kulegeza badala ya kukaza. Enyi kaumu ya Musa! Nitakuonyesheni katika vitabu vyenu makaazi ya wale wanao asi amri za Mwenyezi Mungu, na watavyo angamia, ili mpate kuzingatia. Basi msende kinyume yakakusibuni yalio wasibu hao waasi.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye.
- Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa
- Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu
- Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutashinda.
- Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu
- Basi anaye taka atakumbuka.
- Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
- Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara.
- La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua.
- Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



