Surah Al Imran aya 37 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّهِ ۖ إِنَّ اللَّهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ﴾
[ آل عمران: 37]
Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So her Lord accepted her with good acceptance and caused her to grow in a good manner and put her in the care of Zechariah. Every time Zechariah entered upon her in the prayer chamber, he found with her provision. He said, "O Mary, from where is this [coming] to you?" She said, "It is from Allah. Indeed, Allah provides for whom He wills without account."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
Mwenyezi Mungu alimpokea Maryamu kuwa ni nadhiri aliyo iweka mama yake, akamwitikia maombi yake, akamkuza makuzo mema, na akamlea katika kheri yake, Mola Mlezi, huku akimruzuku na kumshughulikia kwa malezi mazuri ya kumpa nguvu mwili wake na roho yake. Mwenyezi Mungu akamkabidhi Zakariya a.s. awe mlezi wake. Zakariya kila akiingia chumbani, alipo kuwa Maryamu anaabudu, akikuta chakula wasicho kizowea wakati ule. Zakariya akasema kwa kustaajabu: Ewe Maryamu! Umepata wapi riziki hii? Naye akamjibu: Hichi ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu. Ni shani yake kumruzuku mja wake amtakaye riziki nyingi bila ya hisabu au kipimo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Namna hivi ndivyo walivyo geuzwa walio kuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
- Na tukawaokoa walio amini na wakawa wanamcha-mngu.
- Hapana akigusaye ila walio takaswa.
- Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe?
- Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
- Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
- Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila upande, naye wala hafi.
- Wallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako, lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao.
- Na shari ya giza la usiku liingiapo,
- Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers