Surah Hud aya 84 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴾
[ هود: 84]
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And to Madyan [We sent] their brother Shu'ayb. He said, "O my people, worship Allah; you have no deity other than Him. And do not decrease from the measure and the scale. Indeed, I see you in prosperity, but indeed, I fear for you the punishment of an all-encompassing Day.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shuaib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni.
Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao kwa nasaba na mapenzi na kuoneana huruma, Shuaib. Aliwaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu Mmoja peke yake. Nyinyi hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Wala msipunguze vipimo na mizani mnapo wauzia watu vitu vya kupimwa kwa pishi au kwa mizani. Hakika mimi nakuoneni ni watu wa kutarajiwa kheri kwa kumshukuru na kumtii Mwenyezi Mungu, na kuwapa watu haki zao kaamili. Na mimi nakukhofieni ikiwa hamtaishukuru kheri ya Mwenyezi Mungu na hamuitikii amri yake, isije ikakuteremkieni adhabu ya siku msio weza kuvikimbia vitisho vyake, kwa kuwa hivyo huwazinga wanao adhibiwa wasipate njia ya kusalimika. Hizi Aya mbili zinakataza kupunja kwa vipimo na mizani kwa kuwa ni ukhalifu unao stahiki kupewa adhabu na kuaziriwa. Makosa haya ya kupunja na udanganyifu pia yanahisabiwa ni ukhalifu hata katika kanuni za kutungwa za dikrii. Na katika Qurani tukufu ni moja katika njia ya kulinda mali. Nchi ya Madyana ipo baina ya kaskazi ya Hijazi na kusini ya Sham. Na hii ilikuwa imejaa miti. Ikiitwa Al-aykah,(yaani Machakani). Na Mwenyezi Mungu aliwapelekea adhabu kwa sababu ya uasi wao.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.
- Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu
- Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe. Na
- Zitacheka, zitachangamka;
- Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo
- Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
- Kama kwamba hawakuwako huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni!
- Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
- Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
- Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers