Surah Nahl aya 92 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴾
[ النحل: 92]
Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jengine? Hakika Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atakubainishieni Siku ya Kiyama mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And do not be like she who untwisted her spun thread after it was strong [by] taking your oaths as [means of] deceit between you because one community is more plentiful [in number or wealth] than another community. Allah only tries you thereby. And He will surely make clear to you on the Day of Resurrection that over which you used to differ.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jengine? Hakika Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atakubainishieni Siku ya Kiyama mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Wala msiwe katika kwenda kinyume na viapo vyenu baada ya kuvithibitisha mfano wa mwanamke mwendawazimu anaye sokoto sufi, ikisha kuwa nyuzi akazifumua tena. Mkafanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganya na kukhadaa watu, na huku mkijitafutia udhuru kwa kuwa ama nyinyi ni wengi zaidi au mna nguvu zaidi kuliko wao, au mnakusudia kuwaunga mkono maadui wenye nguvu zaidi kuliko wao, au kwa kuwa mnataraji kuzidi nguvu kwa khiana! Na hakika Mwenyezi Mungu anakufanyieni mtihani. Mkikhiari kutimiza ahadi mtapata mavuno ya duniani na Akhera. Mkielekea khiana, basi ni khasara yenu. Na hakika Siku ya Kiyama atakubainishieni ukweli wa khitilafu zenu za duniani, na atakulipeni kwa mujibu wa vitendo vyenu. Aya mbili hizi zinaonyesha kuwa msingi wa makhusiano baina ya Waislamu na wengineo pamoja na uadilifu ni kutimiza ahadi, na kwamba makhusiano baina ya mataifa hayasimami sawa ila kwa kutimiza ahadi, na kwamba dola za Kiislamu zikijifunga kwa mapatano basi zijifunge kwa jina la Mwenyezi Mungu. Maana ya hayo ni kuwa inakuwapo yamini ya Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye ndiye dhamini. Na Aya inafahamisha mambo matatu, ambayo lau kuwa mataifa yangeli yatimiza basi amani ingeli enea: Kwanza: Haifai mapatano kuwa ndio njia ya kufanya khadaa. Ikiwa hivyo inakuwa ni udanganyifu. Na udanganyifu haufai katika makhusiano baina ya wanaadamu, sawa sawa ikiwa baina ya mtu na mtu, au kikundi na kikundi, au baina ya madola. Pili: Kutimiza ahadi peke yake ni nguvu. Na mwenye kuvunja ahadi ni kama mwenye kuvunja alicho kijenga kwa sababu za nguvu. Basi anakuwa kama mpumbavu anaye tatua uzi wake kila akisha usokota. Tatu: Haimfalii mtu kuvunja ahadi kwa sababu ya kutafuta nguvu au kutaka kuzidisha kipande cha ardhi.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!
- Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
- Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni
- Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.
- Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na tamaa. Na hukuteremshieni maji kutoka
- Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kisha
- Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa.
- Na tutawafanya vijana,
- Na hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyo weza kuifikia ila kwa mashaka ya nafsi.
- Wote hao tunawakunjulia - hawa na hao - katika neema za Mola wako Mlezi. Wala
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



