Surah Yusuf aya 50 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ﴾
[ يوسف: 50]
Na mfalme akasema: Mleteni kwangu! Basi mjumbe alipo mjia Yusuf alisema: Rejea kwa bwana wako ukamuulize khabari ya wale wanawake walio jikata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao.
Surah Yusuf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And the king said, "Bring him to me." But when the messenger came to him, [Joseph] said, "Return to your master and ask him what is the case of the women who cut their hands. Indeed, my Lord is Knowing of their plan."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mfalme akasema: Mleteni kwangu! Basi mjumbe alipo mjia Yusuf alisema: Rejea kwa bwana wako ukamuulize khabari ya wale wanawake walio jikata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao.
Mfalme akamwona Yusuf atakuwa na faida naye kwa ule uwezo wake kuifasiri ndoto yake, na akaazimia amwite. Akawaamrisha wasaidizi wake wamlete. Alipo mfikia mjumbe akamwabia kuwa mfalme anamtaka, khabari hiyo haikumpapatisha, juu ya kuwa ina bishara ya kufunguliwa kwake. Wala kule kutamani kutoka kwa mfungwa kwenye dhiki za jela na taabu zake hakukuitikisa subira yake. Akakhiari angoje mpaka idhihirike kuwa hana makosa kuliko kufanya haraka kutoka na huku yale aliyo tuhumiwa bado yamemganda. Akamwambia mjumbe: Rejea kwa bwana wako umtake ayaangalie tena yale mashtaka niliyo shitakiwa, awaulize wale wanawake walio kusanywa na mke wa Mheshimiwa kwa kunifanyia hila mimi, wakababaika na wakajikata mikono yao: Je! Walipo toka kwenye yale majaribio walikuwa wanaamini kuwa mimi sina makosa na safi, au waliniona ni mchafu na mzinifu? Mimi nataka haya ipate kuonekana hakika katika macho ya watu. Ama Mola wangu Mlezi anavijua vyema vitimbi vyao!
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi
- Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,
- Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.
- Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya walio sema: Mwenyezi Mungu ni masikini, na sisi ni
- Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo
- Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu,
- Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
- Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena
- Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema? Hakika makafiri
- Lakini aliikadhibisha na akaasi.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yusuf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yusuf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yusuf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers