وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا(1) Naapa kwa pepo zinazo tawanya, |
فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا(2) Na zinazo beba mizigo, |
فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا(3) Na zinazo kwenda kwa wepesi. |
فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا(4) Na zinazo gawanya kwa amri, |
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ(5) Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli, |
وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ(6) Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. |
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ(7) Naapa kwa mbingu zenye njia, |
إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ(8) Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. |
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ(9) Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. |
قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ(10) Wazushi wameangamizwa. |
الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ(11) Ambao wameghafilika katika ujinga. |
يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ(12) Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? |
يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ(13) Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. |
ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ(14) Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. |
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ(15) Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. |
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ(16) Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. |
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ(17) Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. |
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ(18) Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. |
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ(19) Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. |
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ(20) Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. |
وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ(21) Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? |
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ(22) Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. |
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ(23) Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. |
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ(24) Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? |
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ(25) Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. |
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ(26) Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. |
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ(27) Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? |
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ(28) Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. |
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ(29) Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! |
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ(30) Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. |
۞ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ(31) AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? |
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ(32) Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, |
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ(33) Tuwatupie mawe ya udongo, |
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ(34) Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. |
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ(35) Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. |
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ(36) Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! |
وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ(37) Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. |
وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ(38) Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. |
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ(39) Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! |
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ(40) Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. |
وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ(41) Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. |
مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ(42) Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. |
وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ(43) Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. |
فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ(44) Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. |
فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ(45) Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. |
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ(46) Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. |
وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ(47) Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. |
وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ(48) Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! |
وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ(49) Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. |
فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ(50) Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. |
وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ(51) Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. |
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ(52) Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. |
أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ(53) Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. |
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ(54) Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. |
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ(55) Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. |
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ(56) Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. |
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ(57) Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe. |
إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ(58) Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. |
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ(59) Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. |
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ(60) Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. |