Surah Nisa aya 102 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا﴾
[ النساء: 102]
Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when you are among them and lead them in prayer, let a group of them stand [in prayer] with you and let them carry their arms. And when they have prostrated, let them be [in position] behind you and have the other group come forward which has not [yet] prayed and let them pray with you, taking precaution and carrying their arms. Those who disbelieve wish that you would neglect your weapons and your baggage so they could come down upon you in one [single] attack. But there is no blame upon you, if you are troubled by rain or are ill, for putting down your arms, but take precaution. Indeed, Allah has prepared for the disbelievers a humiliating punishment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
Ewe Nabii Muaminifu, ukiwa nao na Swala ya Jamaa inasaliwa, msisahau kutahadhari na maadui. Na hayo ni kuwagawa Waislamu makundi mawili. Moja lianze kuswali kwa kukufuata wewe, na wakati huo la pili lisimame kwa hadhari na silaha likilinda vifaa. Ukisha nusu ya Swala, kundi lilio sali nawe lende nyuma yako, na lije jengine lisali nawe Swala iliyo bakia. Kisha litimize sehemu waliyo ikosa. Na lile la kwanza lisali baki ya Swala. Na hii huitwa -Laahiqah-, yaani iliyo kutwa na nyengine inaitwa -Masbuuqah-, yaani iliyo tanguliwa ,kwa kuwa inasaliwa mwanzo wa Swala ya Jamaa; na -Laahiqah- inasaliwa mwisho wa Swala ya Jamaa. Mpango huu ni kwa sababu isikosekane Swala, na kutahadhari na makafiri ambao wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu wapate kukuvamieni kwa ghafla, na wakumalizeni nanyi mmo katika Swala. Vita na washirikina ni waajibu, na havina ukomo. Lakini hapana dhambi juu yenu kusita kwa ajili ya udhuru kama mvua au maradhi, juu ya kuwa lazima muwe na hadhari ya kudumu. Na hii ni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa makafiri hapa duniani, na Akhera amewaandalia adhabu ya fedheha na udhalili. -Laahiq- ni anaye swali na Imam mwanzo wa Swala na akalazimika kusali iliyo baki peke yake, na -Masbuuq- anaye iwahi sehemu ya mwisho ya Swala ya Jamaa, kisha akatimiza sehemu aliyo ikosa peke yake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili
- Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni
- Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana
- Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.
- Shungi la uwongo, lenye makosa!
- Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza.
- Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhaahiri.
- Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi
- Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama
- Hao ndio walio waambia ndugu zao na wao wenyewe wakakaa kitako: Lau wengeli tut'ii wasingeli
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers