Surah Nisa aya 135 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا﴾
[ النساء: 135]
Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, be persistently standing firm in justice, witnesses for Allah, even if it be against yourselves or parents and relatives. Whether one is rich or poor, Allah is more worthy of both. So follow not [personal] inclination, lest you not be just. And if you distort [your testimony] or refuse [to give it], then indeed Allah is ever, with what you do, Acquainted.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.
Uadilifu ndio nidhamu ya maumbile. Na hiyo ndiyo sharia ambayo haiwezi kuwapo ndani yake maoni ya kukhitalifiana. Basi enyi mlio mtii Mwenyezi Mungu wa Haki, na wito wa Mitume wake, kuweni macho nafsi zenu katika kuutii uadilifu, na kuweni macho kwa ajili ya watu. Mfanyieni insafu aliye dhulumiwa, na msimame imara, si kwa ajili ya kumpendelea tajiri, au kumwonea huruma masikini. Kwani Mwenyezi Mungu aliye waumba matajiri na masikini anastahiki zaidi kuangalia hali ya tajiri au fakiri. Matamanio ndiyo yanayo mpelekea mtu kumili nafsi yake, basi msiyafuate matamanio mkaacha uadilifu. Na mkikengeuka mkaacha uadilifu, au mkapuuza kusimamisha uadilifu, basi mjue Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo, tena anayajua kwa ujuzi wa ndani. Naye atakulipeni kwa mujibu wa amali yenu; ikiwa njema mtalipwa wema, ikiwa ovu mtalipwa shari.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao ange wasikilizisha, na lau ange wasikilizisha wangeli
- Humo watadumu. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi.
- Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
- Walipo kuwa wamekaa hapo,
- Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
- Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na
- Akasema msemaji kati yao: Msimuuwe Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Wasafiri watakuja mwokota; kama
- Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko
- Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate
- Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers