Surah Anam aya 138 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَقَالُوا هَٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴾
[ الأنعام: 138]
Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And they say, "These animals and crops are forbidden; no one may eat from them except whom we will," by their claim. And there are those [camels] whose backs are forbidden [by them] and those upon which the name of Allah is not mentioned - [all of this] an invention of untruth about Him. He will punish them for what they were inventing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia.
Na katika mawazo yao ni kusema kwao: Ngamia hawa, na ngombe hawa, na mbuzi na kondoo hawa, na mazao haya ya mimea, ni marfuku. Hayali mtu ila wamtakaye katika utumishi wa masanamu. Hayo ni kwa madai yao ya uwongo, wala hayatokani na Mwenyezi Mungu. Na pia husema: Ngamia hawa wameharimishwa migongo yao, basi hapana ruhusa mtu kuwapanda. Nao juu ya hao hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wanapo wachinja hao ngamia, na ngombe, na mbuzi na kondoo. Na hayo ni kwa kule kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ushirikina wao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa adhabu huko Akhera kwa sababu ya uzushi wao, na kuharimisha kwao vitu ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharimisha.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Siku wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake watapo waambia walio amini: Tungojeni ili tupate mwangaza katika
- Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
- Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'ani. Basi walipo ihudhuria walisema:
- Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake:
- Je! Mnauona moto mnao uwasha?
- Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
- Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
- Na hakika amekhasiri aliye iviza.
- Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers