Surah Anam aya 144 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّهُ بِهَٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴾
[ الأنعام: 144]
Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And of the camels, two and of the cattle, two. Say, "Is it the two males He has forbidden or the two females or that which the wombs of the two females contain? Or were you witnesses when Allah charged you with this? Then who is more unjust than one who invents a lie about Allah to mislead the people by [something] other than knowledge? Indeed, Allah does not guide the wrongdoing people."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
.Na wawili katika ngamia, na wawili katika ngombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu.
Na Mwenyezi Mungu ameumba ngamia namna mbili, dume na jike, na ngombe namna mbili mbili vile vile. Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanya: Nini sababu ya kuwaharimisha hao mlio harimisha kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa wao ni madume? Sivyo hivyo; kwa sababu pengine mnahalalisha madume! Au ni kwa kuwa majike? Pia sio hivyo, kwa sababu mnahalalisha majike wakati mwingine! Au kwa kuwa wana watoto matumboni mwao? Pia sio hivyo, kwa sababu hamkuharimisha watoto walio matumboni daima. Nanyi mnadai kuwa kuharimisha huku kunatokana na Mwenyezi Mungu! Nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuharimisheni haya na mkamsikia makatazo yake? Kabisa hayo hayakuwa. Wacheni mlio nayo; kwani hiyo ni dhulma. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko mwenye kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamnasibisha nayo mambo yasiyo toka kwake, wala hayana tegemeo lolote la ki-ilimu la kutegemea, bali huyo anataka kuwapotosha watu tu! Mwenyezi Mungu hawawafikishi wenye kudhulumu wakikhiari njia ya upotovu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
- Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa
- Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba
- Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!
- Na mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tukimwondoshea
- Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
- Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika
- Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
- Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.
- Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



