Surah Anam aya 148 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ﴾
[ الأنعام: 148]
Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Those who associated with Allah will say, "If Allah had willed, we would not have associated [anything] and neither would our fathers, nor would we have prohibited anything." Likewise did those before deny until they tasted Our punishment. Say, "Do you have any knowledge that you can produce for us? You follow not except assumption, and you are not but falsifying."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu.
Kwa kutaka kujitolea udhuru kwa ushiriki wao, na kule kuharimisha vyakula alivyo halalisha Mwenyezi Mungu, na kukanusha yaliyo wafikia kuwa Mwenyezi Mungu kaudhika nao kwa vitendo vyao, washirikina watasema: Ushirikina wetu na kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu, ni kwa mujibu wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuridhi kwake! Na lau angeli penda Yeye kinyume cha hayo, na angeli chukia tuyatendayo, basi tusingeli mshirikisha sisi wala walio tutangulia, na wala tusingeli harimisha kitu chochote alicho tuhalalishia. Na walio kabla yao waliwakadhibisha Mitume wao, kama hawa wanavyo kukadhibisha wewe. Na waliendelea katika kukanusha kwao mpaka ikawafikia adhabu yetu! Waambie hawa wanao kanusha: Jee mnao ushahidi wa kutegemea ulio sahihi ya kwamba Mwenyezi Mungu amekuridhieni nyinyi mumshirikishe na mhalalishe, mkatutolea? Katika maneno yenu hamfuati ila kudhania tu. Na hiyo haitoshelezi chochote katika Haki. Na nyinyi si chochote, si lolote, ila ni waongo tu katika hayo mnayo dai.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.
- Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
- Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu
- Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanashauriana kukuuwa.
- Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni
- Na wakasema: Sisi tuna mali mengi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa.
- Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba
- Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers