Surah Nisa aya 157 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا﴾
[ النساء: 157]
Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [for] their saying, "Indeed, we have killed the Messiah, Jesus, the son of Mary, the messenger of Allah." And they did not kill him, nor did they crucify him; but [another] was made to resemble him to them. And indeed, those who differ over it are in doubt about it. They have no knowledge of it except the following of assumption. And they did not kill him, for certain.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
Na Mwenyezi Mungu pia amewaghadhibikia kwa kusema kwao uwongo: Hakika sisi tumemuuwa Masihi Isa bin Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na kweli ya yakini ni kuwa hawakumuuwa kama wanavyo zua. Wala hawakumsulubu kama wanavyo dai. Lakini walifananishiwa, nao wakadhani kuwa wamemuuwa na wamemsalibu. Na hakika walimuuwa na kumsalibu aliye shabihiana naye. Nao wakaja kukhitalifiana baada ya hayo, kuwa aliyeuwawa ni Isa au mtu mwengine? Na wote hao, kwa hakika, wamo katika shaka tu juu ya jambo hilo. Kweli iliyopo ni kuwa hawana ujuzi nayo mambo haya, ila ni dhana tu. Kabisa hawakumuuwa Isa. (Wataalamu wa Biblia mpaka hii leo wamo kuzozana katika jambo hili. Mwenye kuzichungua Injili zinazo kubaliwa na Wakristo ataona kuwa hazina uthibitisho kuwa aliye salibiwa ndiye Yesu, au hata huyo naye alikufa msalabani au la.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
- Na watoto wanapo fikilia umri wa kubaalighi basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa
- Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,
- Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.
- Walio baki nyuma watasema: Mtapo kwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi
- Enyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakini msihalalishe
- Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
- Katika Siku iliyo kuu,
- Na msivyo viona,
- Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye fafanua baina yao Siku ya Kiyama katika waliyo kuwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers