Surah Raad aya 17 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا فَاحْتَمَلَ السَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًا ۚ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِي النَّارِ ابْتِغَاءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَاعٍ زَبَدٌ مِّثْلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ الْحَقَّ وَالْبَاطِلَ ۚ فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً ۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ﴾
[ الرعد: 17]
Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
He sends down from the sky, rain, and valleys flow according to their capacity, and the torrent carries a rising foam. And from that [ore] which they heat in the fire, desiring adornments and utensils, is a foam like it. Thus Allah presents [the example of] truth and falsehood. As for the foam, it vanishes, [being] cast off; but as for that which benefits the people, it remains on the earth. Thus does Allah present examples.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baatili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano.
Na hakika neema zake Mtukufu mnaziona, na masanamu yenu hayana athari yoyote katika neema hizo. Yeye ndiye anaye kuteremshieni mvua kutoka kwenye mawingu, na mito na mabonde yakamiminika maji, kila kitu kwa kadiri yake aliyo ikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa ajili ya kuzalisha mimea, na matunda ya miti. Na mito inapo miminika hubeba juu yake visio kuwa na manufaa, na huwa katika hivyo vyenye nafuu hubakia, na visio na faida hupita. Mfano wa hayo ni Haki na baatili, kweli na uwongo. Haki hubakia na baatili ikapita. Na katika maadeni yanayo yayushwa kwa moto kwa kufanyia mapambo, kama dhahabu na fedha, na yanayo tumiwa kwa manufaa mengine kama chuma na shaba, kadhaalika sehemu isiyo na faida huwa juu kama povu na hutupwa. Na yenye nafuu ndio hubakia. Kadhaalika katika imani. Potovu hupita, na iliyo ya kweli hubakia. Kwa mfano kama huu Mwenyezi Mungu Subhanahu anabainisha ukweli wa mambo, na hupiganisha mifano hii kwa hii ili yote yabainike wazi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ikigundulikana kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wawili wengineo kutokana na warithi wenye kudai haki
- Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema
- Mna nini? Mnahukumu vipi?
- Na tutawafanya vijana,
- Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya
- Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi tulikuwa hatuna khabari
- Ewe Nabii! Kwa nini unaharimisha alicho kuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi
- Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
- Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
- Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata tija, wala hawakuwa wenye
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers