Surah Raad aya 16 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴾
[ الرعد: 16]
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Say, "Who is Lord of the heavens and earth?" Say, "Allah." Say, "Have you then taken besides Him allies not possessing [even] for themselves any benefit or any harm?" Say, "Is the blind equivalent to the seeing? Or is darkness equivalent to light? Or have they attributed to Allah partners who created like His creation so that the creation [of each] seemed similar to them?" Say, "Allah is the Creator of all things, and He is the One, the Prevailing."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!
Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii wake ajadiliane na washirikina kwa kuwaongoa na kuwabainishia. Akamwambia: Ewe Nabii! Waambie: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi, naye ndiye Mwenye kuzilinda, na Mwenye kuviendesha viliomo humo? Tena uwaeleze jawabu iliyo sawa hiyo wanayo ishindania. Waambie: Huyo ni Mwenyezi Mungu anaye abudiwa kwa haki, hana mwenginewe. Basi ni waajibu wenu mumuabudu Yeye peke yake. Tena waambie: Mnaziona dalili zilizo thibiti zinazo onyesha uumbaji wake kila kitu peke yake? Na juu ya hivyo mnawafanya masanamu kuwa ni miungu, bila ya kukubali kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja! Na haya masanamu hayajifai wenyewe kheri wala shari! Vipi basi mnayafanya sawa na Muumba Mwenye kupanga? Nyinyi mnafanya sawa baina ya Muumba wa kila kitu na asiye miliki kitu! Mmekuwa kama anaye fanya sawa baina ya viwili vinavyo gongana! Basi hebu ni sawa baina ya mwenye kuona na asiye ona? Je, giza totoro na mwangaza unao ngaa ni sawa? Je, usawa huo unaingia akilini mwao? Au upotovu wao umepita hadi hata wanadai kuwa hayo masanamu yao ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika kuumba na kupanga, hata yakawadanganyikia wasijue mambo ya uumbaji, kama walivyo potea katika kuabudu? Waambie ewe Nabii! Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Muumba wa kila kiliopo. Na Yeye ni peke yake katika kuumba na kuabudiwa, Mwenye kushinda kila kitu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu
- Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
- Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.
- Na pale alipo tangaza Mola wako Mlezi kwamba hapana shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa
- Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake,
- Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha
- (Musa) akasema: Hayo ndiyo tuliyo kuwa tunayataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyo jia.
- Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers