Surah Nisa aya 176 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾
[ النساء: 176]
Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
They request from you a [legal] ruling. Say, "Allah gives you a ruling concerning one having neither descendants nor ascendants [as heirs]." If a man dies, leaving no child but [only] a sister, she will have half of what he left. And he inherits from her if she [dies and] has no child. But if there are two sisters [or more], they will have two-thirds of what he left. If there are both brothers and sisters, the male will have the share of two females. Allah makes clear to you [His law], lest you go astray. And Allah is Knowing of all things.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Ewe Nabii! Wanakuuliza vipi atarithiwa aliye kufa naye akawa hana mwana, wala mzazi. Sema: Hakika hukumu ya Mwenyezi Mungu katika urithi wa hawa ni kuwa, akiwa maiti ana ndugu wa kike basi atapata nusu ya tirka. Na akiwa maiti ni mwanamke naye ana ndugu wa kiume basi atarithi mali yote. Na ikiwa ameacha ndugu wawili wa kike, basi watapata hao thuluthi mbili ya urithi. Na ikiwa hao ndugu ni mchanganyiko wanaume na wanawake, basi fungu la mwanamume ni sawa na mafungu mawili ya wanawake. Mwenyezi Mungu anakubainishieni haya msije mkapotea katika kugawa mafungu ya urithi. Na Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu wa ujuzi wa amali zenu na vitendo vyenu vyote. Na atakulipeni kwavyo. (Angalia: Urithi wa ndugu katika Aya hii ni wa ndugu khalisa, yaani ndugu kwa baba na mama, au ndugu kwa baba. Ama urithi wa ndugu kwa mama tu umekwisha tajwa katika Aya 12 ya Sura hii ya Annisaa.) Na Sunna (Mafunzo ya Mtume) imebainisha kuwa wakizidi kuliko ndugu wa kike wawili, pamoja na Aya ya mirathi iliyo tajwa, kuwa wakizidi kuliko binti wawili, watachukua thuluthi mbili. Ni bora kuwa zaidi kuliko ndugu wawili wa kike, kwa sababu mabinti ni karibu zaidi kwa maiti. Tuzingatie kuwa kwa mujibu wa kanuni za Kizungu za kurithi, ambazo zimetokana na kanuni ya Kirumi, ndugu wanaume wala wa kike wala watoto wao hawarithi. Na juu ya hivyo mwenye mali anayo ruhusa kumkata yeyote asipate urithi wake. Uislamu umekataza haya. Warithi lazima wapate urithi wao, ila mtu anayo haki ya kuandika wasia kujihukumia kisicho zidi thuluthi moja ya mali yake.(W.H. Ingrams katika kitabu chake Zanzibar Its History and Its People ameandika: -Hakika Sharia Takatifu yaonekana kuwa ni ya haki zaidi sana kuliko hata mpango wa Kiingereza wa kugawanya mali. Katika Zanzibar [na bila ya shaka katika Waislamu wote] hapana mwendo wa kuwa mtu -kukatwa urithi akabakishwa na shilingi moja tu-; vyo vyote vile, ni sehemu ndogo tu ndiyo inaweza kuandikiwa wasia, na yaliyo baki lazima yagawiwe kwa warithi kwa mujibu wa kiwango maalumu.-)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Alikunja kipaji na akageuka,
- Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala
- Literemshalo linyanyualo,
- Basi litapo pulizwa barugumu,
- Ingieni kwenye milango ya Jahannamu, mdumu humo milele. Basi ni maovu yaliyoje makaazi ya wanao
- Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
- Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani, kabla haujamalizika ufunuo wake.
- Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na watu mafisadi hawa!
- Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini
- Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache Njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers