Surah Ahqaf aya 21 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴾
[ الأحقاف: 21]
Na mtaje ndugu wa kina A'di, alipo waonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: Msimuabudu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nakukhofieni isikupateni adhabu ya siku iliyo kuu.
Surah Al-Ahqaaf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And mention, [O Muhammad], the brother of 'Aad, when he warned his people in the [region of] al-Ahqaf - and warners had already passed on before him and after him - [saying], "Do not worship except Allah. Indeed, I fear for you the punishment of a terrible day."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mtaje ndugu wa kina Adi, alipo waonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: Msimuabudu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nakukhofieni isikupateni adhabu ya siku iliyo kuu.
Mtaje Hud, mwenzao kabila ya Adi, alipo wahadharisha watu wake wanao kaa Ahqaaf, kwenye vilima vya mchanga. Na Mitume kadhaa walikuja kabla yake na baada yake kwa maonyo kama yake ya kusema: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu. Mimi nakukhofieni isikupateni adhabu yenye vitisho vikuu. Maskani ya kabila hii ilikuwa huko Ahqaaf, kwenye vilima vya mchanga. Na wapi hapo Ahqaaf? Zipo khitilafu. Baadhi ya wanazuoni wa taarikh (historia) wanasema kuwa hapo ni baina ya Yaman na Oman mpaka Hadhramaut na Shihr, yaani mashariki ya kusini ya Bara Arabu. Na baadhi ya wachunguzi wa zama za karibu wanaona ni mashariki ya aqaba, wakitegemea maandishi ya Nabatia waliyo yakuta katika magofu ya hekalu walilo livumbua katika mlima wa Arim. Walikuta pembezoni mwa mlima huo mabaki ya siku za Jahiliya za zamani. Wakasahihisha kuwa hapo ndipo ilipo Arim iliyo tajwa katika Qurani tukufu. Kisha kabila hiyo ikatoka hapo kabla ya Uislamu, na hapana kilicho baki chao isipo kuwa chemchem ya maji ambayo wafanyi biashara na watu wa misafara wakishukia hapo katika njia yao kwendea Shamu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
- Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
- Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni?
- Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye
- Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora.
- Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
- Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.
- Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa
- Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
- Na mimea na vyeo vitukufu!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Ahqaf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Ahqaf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Ahqaf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers