Surah Baqarah aya 219 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ﴾
[ البقرة: 219]
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri--
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
They ask you about wine and gambling. Say, "In them is great sin and [yet, some] benefit for people. But their sin is greater than their benefit." And they ask you what they should spend. Say, "The excess [beyond needs]." Thus Allah makes clear to you the verses [of revelation] that you might give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri--
Ewe Muhammad! Wanakuuliza juu ya hukumu ya ulevi na kamari. Waambie kwamba katika yote mawili hayo pana madhara makubwa, kwa kuharibu siha na kupoteza akili na mali, na kuleta chuki na uadui baina ya watu. Pia ndani ya hayo yapo manufaa, kama kujipumbaza na kupata faida ya sahali. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake, basi epukaneni nayo. Na wanakuuliza watoe nini? Wajibu watoe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kilicho chepesi na hakina uzito kukitoa. Hivyo ndio Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri yale yatakayo kurejeeni katika maslaha ya dunia na Akhera. Kifungu hichi cha Qurani kinatuwekea wazi makusudio ya sharia ya Kiislamu. Kinatueleza kuwa sharia inataka manufaa ya waja. Chenye kuzidi nafuu yake kuliko madhara kinafaa. Chenye nafuu chache kuliko madhara kinakatazwa. Pia kifungu kinatuonyesha kuwa vitu ulimwenguni vimechanganya mema na mabaya. Hapana ovu lisio kuwa na wema, wala wema usio na uovu. Ulevi, mama wa maovu, unao haribu akili na kumfanya mtu kuwa mnyama, nao una faida pamoja na uovu wake usio na mpaka. Na kamari inayo shughulisha nafsi na akili, ikaleta mpapatiko usio sita, nayo ina nafuu yake pamoja na kuwa na madhambi yanayo fisidi maisha na nyumba za watu, na kila makhusiano bora ya binaadamu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
- Na hao watu wa Mnyanyukoni watawaita watu wanao wajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu
- Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi
- Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini bila ya
- Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
- Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu
- Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na
- Akasema: Hebu nambie khabari ya huyu uliye mtukuza juu yangu. Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Kiyama,
- Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa
- Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers