Surah Baqarah aya 221 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ﴾
[ البقرة: 221]
Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And do not marry polytheistic women until they believe. And a believing slave woman is better than a polytheist, even though she might please you. And do not marry polytheistic men [to your women] until they believe. And a believing slave is better than a polytheist, even though he might please you. Those invite [you] to the Fire, but Allah invites to Paradise and to forgiveness, by His permission. And He makes clear His verses to the people that perhaps they may remember.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.
Hapana ubaya wowote kuchanganyika na mayatima, lakini kuchanganyika na washirikina ni vibaya. Muumini hana ruhusa kumwoa mshirikina asiye fuata dini ya Kitabu cha mbinguni. Basi msipelekewe kutaka kumwoa mwanamke wa kishirikina kwa ajili ya mali yake, au uzuri wake, au jaha yake, au ukoo wake. Muumini aliye mtumwa ni bora kuliko mshirikina aliye huru mwenye mali, na jamali, na utukufu na nasaba. Wala nyinyi msiwaoeze wanawake walio mikononi mwenu wanaume wa kishirikina wasio amini Vitabu vya mbinguni, wala yasikupelekeeni kumkhiari mshirikina utajiri na cheo chake. Mtumwa Muumini ni bora kuliko huyo. Hao washirikina wanawavutia wenzao kwenda katika maasi na ushirikina, na kwa hivyo wanapaswa kuingia Motoni. Na Mwenyezi Mungu anapo kulinganieni mjitenge na ndoa za washirikina anakulinganieni kwa ajili ya maslaha yenu na mwongoke ili mpate Pepo na maghfira, na mwende katika njia ya kheri kwa taisiri. Na Mwenyezi Mungu anabainisha sharia zake na uwongofu wake kwa watu wapate kujua maslaha yao na kheri yao.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
- Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae
- Na atendaye kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika dhulma na dhambi
- Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
- Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani. Subira ni njema! Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea
- Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika
- Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila
- Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
- Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo,
- Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema: Ewe Musa!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers