Surah Baqarah aya 222 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ﴾
[ البقرة: 222]
Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And they ask you about menstruation. Say, "It is harm, so keep away from wives during menstruation. And do not approach them until they are pure. And when they have purified themselves, then come to them from where Allah has ordained for you. Indeed, Allah loves those who are constantly repentant and loves those who purify themselves."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watahirike. Wakisha tahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.
Na wanakuuliza juu ya kuwaingilia wake zenu wakati wanapo kuwa na damu ya mwezi, hedhi. Waambie kuwa hedhi ni uchafu. Basi jizuieni kuwaingilia wakati wake mpaka watahirike (wasafike). Wakitahirika basi ingianeni nao katika njia za maumbile. Na ikiwa mtu amefanya makosa katika haya, basi na atubu, na Mwenyezi Mungu anapenda waja wake wakithiri toba na usafi kutokana na uchafu. Ilimu ya kisasa zimethibitisha kuwa wakati wa hedhi yanaweza kuwa madhara kwa kuwa zalio huweza kupata maradhi pindi likiingiliwa na vidudu vya maradhi, ambavyo ni vyepesi kuingia wakati wa kuingiliana na mwanamume. Maradhi hayo huenda yakasababisha mwanamke asiweze kuzaa. Mwanamume naye huambukia maradhi hayo kutokana na mwanamke kwa kupitia njia za mkojo, na maradhi yakapanda juu mpaka mafigo yakaharibika, na kuathirika vyombo vya uzazi, na mwanamume naye akawa hawezi kutia mimba. Maradhi haya huleta machungu makubwa. Watu walikuwa hawajui, lakini Mwenyezi Mungu anajua kila kitu. Na mwanamke anapo kuwa na damu anakuwa hana raghba ya kuingiliwa, basi kumuingilia wakati huo huenda kukamletea hali ya nafsi mbaya na chuki kwa jambo hilo.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni
- Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu; na ni
- Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
- Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na
- Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani ni
- Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa
- Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika
- Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?
- Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini
- Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



