Surah Baqarah aya 253 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ﴾
[ البقرة: 253]
MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Those messengers - some of them We caused to exceed others. Among them were those to whom Allah spoke, and He raised some of them in degree. And We gave Jesus, the Son of Mary, clear proofs, and We supported him with the Pure Spirit. If Allah had willed, those [generations] succeeding them would not have fought each other after the clear proofs had come to them. But they differed, and some of them believed and some of them disbelieved. And if Allah had willed, they would not have fought each other, but Allah does what He intends.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.
Hao ni Mitume ambao baadhi yao tumewataja, wengine tumewatukuza kuliko wenginewe. Wamo kati yao walio semezwa na Mwenyezi Mungu ana kwa ana, kama Musa. Na wengine kati yao Mwenyezi Mungu amewanyanyua kushinda vyeo vya wote, kama Muhammad ambaye akamkhusisha kumpa Ujumbe kwa ulimwengu wote, na kukamilisha Sharia, na kuwa ni Mtume wa mwisho. Na miongoni mwao ni Isa bin Maryam, ambaye Mwenyezi Mungu alimtia nguvu kwa kumpa miujiza kama kufufua wafu, na kuponyesha upofu na ukoma, na akamletea Jibril, Roho Mtakatifu, ili kumtia nguvu. Na Mitume hawa wameleta Uwongofu, na Dini ya Haki, na Ushahidi ulio wazi wenye kuongoa. Kwa haya imewajibikia watu wote wawaamini, wala wasikhitalifiane, wala wasipigane. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasipigane hao watu baada ya kuletewa Mitume na ishara zilizo wazi zenye kuonyesha Haki, pasingetokea kupigana wala kukhitalifiana. Lakini Mwenyezi Mungu hakutaka hayo. Kwa hivyo wakakhitalifiana. Basi kati yao wakawapo walio amini, na wengine walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli uwana wala wasingeli khitalifiana. Bali wangeli kuwa wote katika Haki. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda apendalo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamngu.
- Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya
- Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni
- Na tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi
- Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
- Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.
- Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
- Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye
- Na Mwenyezi Mungu alipo kuahidini kuwa moja katika makundi mawili ni lenu. Nanyi mkapenda lisilo
- (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers