Surah Baqarah aya 255 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴾
[ البقرة: 255]
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah - there is no deity except Him, the Ever-Living, the Sustainer of [all] existence. Neither drowsiness overtakes Him nor sleep. To Him belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. Who is it that can intercede with Him except by His permission? He knows what is [presently] before them and what will be after them, and they encompass not a thing of His knowledge except for what He wills. His Kursi extends over the heavens and the earth, and their preservation tires Him not. And He is the Most High, the Most Great.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.
Mwenyezi Mungu ndiye anaye stahiki kuabudiwa pekee. Yeye ndiye Mwenye kubaki, Mwenye kuyasimamia mambo ya viumbe daima. Haghafiliki kabisa, wala hanyongonyei, wala halali wala yanayo fanana na hayo, kwani Yeye hasifiki na upungufu wa chochote. Yeye pekee ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi, wala hana mshirika yeyote katika hayo. Kwa hivyo hapana kiumbe anaye weza kumwombea mwenginewe ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Yeye Subhanahu wa Taala anajua kila kitu. Anayajua yaliyo kuwa na yatayo kuwa. Hapana mtu anaye weza kujua kitu katika ilimu ya Mwenyezi Mungu ila atakavyo Yeye ajue na aridhie. Utawala wake umeenea mbinguni na ardhini. Hayamhangaishi Yeye kuyadabiri hayo, kwani Yeye ametukuka, hana upungufu wala kushindwa na jambo, Muadhamu katika utukufu wake na utawala wake. Katika haya upo ushahidi wa kuonyesha ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa daima, na Kusimamia kwake kusio koma kwa yote ya mbinguni na duniani. Pia pana ishara ya kuwa Mwenyezi Mungu hapitikiwi na vituko vinavyo zuka.Ilimu ya Sayansi imethibitisha kuwa kulala ni katika sifa ya wanyama na mimea iliyo hai. Ikiwa Mwenyezi Mungu halali basi Yeye ni hai kwa uhai ulio elekeana na dhati yake, lakini sio kama vilivyo hai vinginevyo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu
- Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli
- Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
- Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na
- Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
- Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu
- Huwaoni wanao fanya unaafiki wanawaambia ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na
- Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ndege wakikunjua mbawa
- Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda
- Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers