Surah Baqarah aya 199 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾
[ البقرة: 199]
Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha: hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then depart from the place from where [all] the people depart and ask forgiveness of Allah. Indeed, Allah is Forgiving and Merciful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha: hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Makureshi walikuwa hawasimami na watu wengine katika Arafat juu ya kuwa wakijua kuwa baba yao Ibrahim akisimama hapo. Na hayo ni kwa kujitukuza wasiwe sawa na wengineo na hali wao ati ni watu wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na ni wakaazi wa katika pahala patakatifu. Wakidai kuwa hayo ni kuitukuza Makka wasitoke kwenda Arafat ambako si kutakatifu kama Makka. Mwenyezi Mungu akawalazimisha wazingolee mbali hizo ada za kijinga, na wasimame katika Arafat, na watoke huko kama watokavyo watu wote. Kwani hapana yeyote aliye bora kuliko mwengine katika utendaji wa ibada. Na inawapasa wamwombe Mwenyezi Mungu maghfira katika mwahala humu mwenye baraka. Hayo ndiyo yana maelekeo zaidi Mwenyezi Mungu kuwasamehe dhambi na makosa yao, na akawarehemu kwa fadhila yake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake
- Na hakika wewe una tabia tukufu.
- Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua!
- Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
- Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye atakuonyesheni Ishara zake,
- Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
- Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
- Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao.
- Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria
- Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers