Surah Raad aya 33 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَفَمَنْ هُوَ قَائِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۗ وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ قُلْ سَمُّوهُمْ ۚ أَمْ تُنَبِّئُونَهُ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي الْأَرْضِ أَم بِظَاهِرٍ مِّنَ الْقَوْلِ ۗ بَلْ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مَكْرُهُمْ وَصُدُّوا عَنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ﴾
[ الرعد: 33]
Je! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyo yachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa khabari ya yale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu? Bali walio kufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha apotee basi hana wa kumwongoa.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then is He who is a maintainer of every soul, [knowing] what it has earned, [like any other]? But to Allah they have attributed partners. Say, "Name them. Or do you inform Him of that which He knows not upon the earth or of what is apparent of speech?" Rather, their [own] plan has been made attractive to those who disbelieve, and they have been averted from the way. And whomever Allah leaves astray - there will be for him no guide.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyo yachuma? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa khabari ya yale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu? Bali walio kufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha apotee basi hana wa kumwongoa.
Hakika washirikina wamefanya upumbavu katika kukanya kwao, wakamfanyia Mwenyezi Mungu washirika wa kuwaabudu. Kwani ati huyo ambaye ndiye Mwenye kuhifadhi na kuangalia kila nafsi, na kuipimia kwa kuilipa kheri na shari inayo ichuma, atakuwa wa kufananishwa na haya masanamu? Ewe Nabii! Waambie: Yaelezeni yalivyo kweli! Je, hayo masanamu ya hai? Yanaweza kujikinga na madhara? Yakiwa mawe hayanufaishi wala hayadhuru, basi mbona mnajidanganya nafsi zenu kuwa miungu hiyo ndio imemwambia Mwenyezi Mungu hayo ambayo mnadhani kuwa Yeye hayajui ya ardhi hii? Au mnaiweka kwenye cheo cha kuiabudu kwa maneno yanayo toka katika ndimi zenu? Hakika iliyopo ni kuwa watu hawa wamezugwa na mazingatio yao na mawazo yao ya upotovu. Na kwa sababu hiyo wameiacha Njia ya Haki wakabaki wakitanga tanga! Na wenye kupotea kama hao, basi hawana wa kuwaongoa yeyote, kwani wameziachisha nafsi zao Njia ya Uwongofu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakuleteeni mbingu zenye
- Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla
- Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
- Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi!
- Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala
- Katika ngozi iliyo kunjuliwa,
- Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
- Na kwa mwezi unapo pevuka,
- Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu
- Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers