Surah An Nur aya 40 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَوْ كَظُلُمَاتٍ فِي بَحْرٍ لُّجِّيٍّ يَغْشَاهُ مَوْجٌ مِّن فَوْقِهِ مَوْجٌ مِّن فَوْقِهِ سَحَابٌ ۚ ظُلُمَاتٌ بَعْضُهَا فَوْقَ بَعْضٍ إِذَا أَخْرَجَ يَدَهُ لَمْ يَكَدْ يَرَاهَا ۗ وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ﴾
[ النور: 40]
Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.
Surah An-Nur in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Or [they are] like darknesses within an unfathomable sea which is covered by waves, upon which are waves, over which are clouds - darknesses, some of them upon others. When one puts out his hand [therein], he can hardly see it. And he to whom Allah has not granted light - for him there is no light.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.
Na huu mfano mwengine wa vitendo vya makafiri. Mfano wake ni mfano wa giza la bahari kubwa iliyo tanda yenye kina kirefu. Mawimbi yake yanapigana na kusukumana wenyewe kwa wenyewe. Nayo yamefunikwa na mawingu mazito meusi hayapitishi mwangaza. Katika giza hili lililo rundikana msafiri wa baharini hawezi kuuona mkono wake hata akiukurubisha machoni. Basi anabaki ameduwaa amebabaika hajijui. Na vipi ataona kitu atokane na butaa hili bila ya kupata Nuru ya kumwongoa katika mwendo wake, na kumwokoa na kugongana na kuhiliki. Na basi kama hali hiyo hiyo makafiri hawapati faida katika vitendo vyao, wala hawatoki katika upofu wao na upotovu wao, wala hawajiokoi nafsi zao, ila kwa Nuru ya Imani. Kwani hana Nuru ya kumwongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. Basi atakuwa katika walio teketea. -Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.- Sarabi si chochote ila mandhari ya mwangaza yanayo sabibishwa na marejeo (reflection) ya miale inayo toka kwenye vitu vyenye kutoa mwanga. Na hiyo hurejeshwa tena kutokana na ardhi pana tupu, yaani uwanda, na kupanda kidogo kidogo mkabala na uso wa ardhi, na joto linapo panda wakati wa mchana, basi miale hiyo inayo rejea ikifika kwa jicho la mwenye kuangalia huona vile vitu vimegeuka juu chini kama kwamba kwenye kiyoo kikubwa kilicho tanda. Na kadhaalika mbingu safi ya rangi ya kibuluu huonekana kama kwamba ni ziwa la maji juu ya uso wa ardhi. Na vile vitu vingine kama miti miti na mitende iliyo onekana juu chini inazidi kuonyesha kama kwamba ni vivuli kwenye maji. Na hii Sarabi huzidi kudhihiri kwa uwazi kabisa inapo kuwa khitilafu ni kubwa baina ya joto la uso wa ardhi na angani katika hewa. Na hayo huonekana zaidi majangwani na nyandani na kwenye barabara za jangwani za lami zilio nyooka. Kwa maelezo hayo inaonekana kuwa Sarabi ni kiini macho tu. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 40: - Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.- Aya hii tukufu imekusanya yaliyo muhimu kabisa katika midharuba ya baharini. Ni maarufu kuwa midharuba ya bahari kuu huwa na mawimbi yanayo khitalifiana urefu wao na ukubwa wao au mnyanyuko wao, hata inaonekana kama kwamba hayo mawimbi yanapandana moja juu ya mwenzie, na kwa hivyo yakaziba mwangaza wa jua kwa vile hiyo midharuba inasabibisha kurundika kwa mawingu mazito ambayo nayo huuziba mwangaza wa jua, na kwa hivyo husabibisha giza mtu asiweze kuona kitu juu ya kuwa macho yake mazima. Na ilivyo kuwa Mtume s.a.w. kazaliwa na kakulia jangwani, kuja maelezo kama haya ya undani ya ki-ilimu kwa ulimi wake kuwa ni ufunuo ulio tokana na Mwenyezi Mungu, ni ushahidi kuwa Qurani inatoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa ni muujiza wa Mtume huyu mtukufu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na anawaitikia wanao amini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na
- Lau kama wangeli pata pa kukimbilia au mapango au pahala pa kuingia basi wangeli fyatuka
- Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la
- Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
- Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni
- Penye Mkunazi wa mwisho.
- Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
- Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
- Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi
- Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah An Nur with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah An Nur mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Nur Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers