Surah An Nur aya 39 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئًا وَوَجَدَ اللَّهَ عِندَهُ فَوَفَّاهُ حِسَابَهُ ۗ وَاللَّهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴾
[ النور: 39]
Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Surah An-Nur in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But those who disbelieved - their deeds are like a mirage in a lowland which a thirsty one thinks is water until, when he comes to it, he finds it is nothing but finds Allah before Him, and He will pay him in full his due; and Allah is swift in account.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Na hao walio pinga na wakakanya wanadhani wenyewe kuwa wamefanya vizuri, na kwamba vitendo vyao vizuri vitawaletea faida Siku ya Kiyama. Lakini hao wamekosea katika dhana yao hiyo. Kwani mfano wa vitendo vyao katika upotovu wake na kukosa maana ni kama mmetuko unao tokea unapo angukia mwako wa jua wakati wa adhuhuri juu ya ardhi tambarare jangwani. Mwenye kiu hudhania kuwa ni maji. Hata akiyafikia asikute chochote chenye manufaa kama alivyo dhania. Hali kadhaalika vitendo vya makafiri siku ya malipo vitakuwa vumbi lilio tawanyika. Na kafiri ataikuta adhabu ya Mwenyezi Mungu inamngojea kwa utimilivu wake bila ya nuksani. Hakika hisabu ya Mwenyezi Mungu hapana shaka inakuja. Na Yeye, Aliye takasika, ni Mwepesi katika kuhisabu kwake, hachelewi wala hakosei.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na kwa mwezi unapo lifuatia!
- Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
- Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
- Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao.
- Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
- Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa.
- Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi
- Na siku hiyo tutawaacha wakisongana wao kwa wao. Na baragumu litapulizwa, na wote watakusanywa pamoja.
- Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.
- Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah An Nur with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah An Nur mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Nur Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



