Surah An Nur aya 43 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يُزْجِي سَحَابًا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيْنَهُ ثُمَّ يَجْعَلُهُ رُكَامًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مِن جِبَالٍ فِيهَا مِن بَرَدٍ فَيُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ وَيَصْرِفُهُ عَن مَّن يَشَاءُ ۖ يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ يَذْهَبُ بِالْأَبْصَارِ﴾
[ النور: 43]
Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.
Surah An-Nur in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Do you not see that Allah drives clouds? Then He brings them together, then He makes them into a mass, and you see the rain emerge from within it. And He sends down from the sky, mountains [of clouds] within which is hail, and He strikes with it whom He wills and averts it from whom He wills. The flash of its lightening almost takes away the eyesight.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.
Ewe Nabii! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu huyavuta mawingu, kisha huyakusanya na kuyarindika moja juu ya moja. Utaona mvua inatoka kwenye mawingu. Na Mwenyezi Mungu huteremsha kutokana na mawingu yaliyo rindikana yanayo shabihi milima kwa ukubwa wake, vipande vya barafu kama changarawe, vikawaangukia watu vikawaletea manufaa au madhara, kufuatana na kanuni zake na matakwa yake, wala asiwateremshie wenginewe kwa mujibu apendavyo Yeye Subhanahu, Mtendaji, Mwenye kukhitari. Mwangaza wa umeme unao tokea kwa kugongana mawingu hukaribia kutia upofu kwa ukali wake. Na mambo kama haya ya kuonekana ni dalili za kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu ambao unao wajibisha kuleta Imani ya kumuamini Yeye. Hajui kushabihiana baina ya mawingu na milima ila mwenye kupanda ndege (eropleni) inayo ruka juu ya mawingu, akayaona kutoka huko juu kama ni milima na vilima. Ilivyo kuwa ndege hizo hazijawa bado zama za Mtume s.a.w. basi hii inakuwa ni dalili kuwa maneno haya yanatokana na Mwenyezi Mungu anaye jua ya juu na chini. -Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.- Aya hii tukufu imeutangulia msafara wa sayansi. Kwani hii yaeleza daraja za kuundika mawingu yanayo rindikana, na sifa zake, na yaliyo juulikana hivi karibuni ki-sayansi ya kwamba mawingu ya mvua huanzia kwa sura ya moja moja kisha yakajumuika yakawa kikundi, ndiyo hayo mawingu yaliyo rindikana, yaani mawingu yanayo endelea kukua kwa kuelekea utosini. Hayo hukua kimo chake hata kufikia urefu wa kilomita 15 au 20, na hapo huonekana kama ni milima mikubwa iliyo nyanyuka. Na yajuulikanayo ki-sayansi ni kuwa mawingu yaliyo rindika yanapitia daraja tatu, nazo: Daraja ya kukusanyika na kukua. Daraja ya kunyesha. Na mwisho daraja ya kumalizikia. Kama ilivyo kuwa mawingu hayo - nayo ni peke yao - yenye mvua ya mawe na inabeba nguvu za umeme (electricity, Kahrabaa) , huweza kuwa yakashika mfululizo wa umeme na radi, hata huweza ikawa ni miripuko karibu 40 kwa dakika moja, hata mtu anaye tazama akawa hawezi tena kuona kwa ukali wa mwanga wake. Na haya ndiyo khasa yanayo wapata marubani wa meli na ndege wakati wa midharuba ya radi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu. Basi tutenge
- Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale walio zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu,
- Nyinyi na baba zenu wa zamani?
- Sema: Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia.
- Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa.
- Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu.
- Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazi bora na mahali penye starehe nzuri.
- Je! Wanaaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au haitawafikia Saa ya Kiyama
- Na waheshimiwa walio kufuru katika kaumu yake wakasema: Mkimfuata Shua'ib, basi hakika hapo nyinyi mtakuwa
- Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah An Nur with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah An Nur mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter An Nur Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers