Surah Araf aya 54 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴾
[ الأعراف: 54]
Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, your Lord is Allah, who created the heavens and earth in six days and then established Himself above the Throne. He covers the night with the day, [another night] chasing it rapidly; and [He created] the sun, the moon, and the stars, subjected by His command. Unquestionably, His is the creation and the command; blessed is Allah, Lord of the worlds.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Hakika Mola Mlezi wenu ambaye Mitume wake wanakuiteni mwende kwenye Haki, na kuiamini Siku ya Mwisho na Malipo, ndiye Muumba ulimwengu, naye ndiye aliye uanza. Kaumba mbingu na ardhi kwa viwango sita, vinavyo shabihiana na siku sita, katika siku za dunia. Kisha akatawala juu ya Ufalme ulio kamilika. Naye ndiye anaye ufanya usiku uufunike mchana kwa kiza chake, na usiku unafuatia mchana kwa upesi na mpango na kufuatana kusikosita, kama anavyo taka Yeye. Naye Mwenyezi Mungu Subhana ameliumba jua, na mwezi, na nyota. Na vyote hivyo vinamnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu, vinakwenda kwa amri yake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kuumba na Mwenye amri ya kuitikiwa. Baraka za Mwenye kuanzisha ulimwengu na viliomo ndani yake zimetukuka. Aya hii tukufu imekusanya maana tatu: Ya kwanza ni kuwa mbingu na ardhi ameziumba Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo siku sita. Na hizi siku sio muradi wake hizi tuzionazo sasa, na tunazo zihisabu. Bali muradi wake ni kubadilika hali, baina ya giza totoro, na giza-giza la alfajiri, na mpambazuko wa asubuhi, na mchana, na adhuhuri, na jioni. Na haya yamekusanya hali sita zinazo badilika. Na giza-giza la magharibi linakitangulia kiza cha usiku. Na hizo hali sita au vipindi sita, ambavyo vimeitwa -siku- ndivyo wanavyo vitaja wanachuoni wa sayansi, navyo ni: Kipindi cha -Ether-, kilicho elezwa katika Surat Ad-dukhan ya 44 ya kuwa ni moshi. Kisha kutokana na hiyo -Ether- yakatokea majua, ambayo moja lake ni hili jua letu. Kisha kutokana na jua zikawa sayari, na miongoni mwa sayari hizo ni hii dunia yetu. Tena katika ardhi zikawamo maadini mbali mbali. Tena ndio kikawa kipindi cha Ardhi, na baadae ukatokea uhai juu yake. Maana ya pili ya Aya hii ni kuwa kila kiliomo ulimwenguni kimo chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu peke yake, wala hapana ufalme usipo kuwa wake Yeye. Na nguvu zozote anazo pewa mtu hatoweza kuuendesha ulimwengu atakavyo. Ukomo wa uwezo wake ni kunufaika na vilivyo umbwa na akajua baadhi ya siri ziliomo ulimwenguni ambazo zilikuwa zimefichika. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliye tuwa na kutawala juu ya Arshi iliyo juu ya vyote vilivyo umbwa, na kwamba nyota na vitu vyote haviendi ila kwa amri yake peke yake. Maana ya tatu ni kuwa kupishana usiku na mchana kumetokea baada ya kwisha umbwa ardhi na mbingu. Basi hizo ni hali zenye kukhusika na asli ya uumbaji wa dunia, na makhusiano ya baina mbingu na ardhi na kuzunguka kwao na Mwenyewe Subhana Mwenye kuumiliki ufalme na utukufu na ukarimu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake,
- Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa
- Basi hakikuwa kilio chao ilipo wafikia adhabu yetu, isipo kuwa kusema: Hakika sisi tulikuwa wenye
- Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
- Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
- Tena wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwashirikisha
- Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Mwenyezi
- Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini.
- Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao?
- Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers