Surah Al Imran aya 7 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ﴾
[ آل عمران: 7]
Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
It is He who has sent down to you, [O Muhammad], the Book; in it are verses [that are] precise - they are the foundation of the Book - and others unspecific. As for those in whose hearts is deviation [from truth], they will follow that of it which is unspecific, seeking discord and seeking an interpretation [suitable to them]. And no one knows its [true] interpretation except Allah. But those firm in knowledge say, "We believe in it. All [of it] is from our Lord." And no one will be reminded except those of understanding.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.
Na Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuteremshia wewe, Muhammad, hii Qurani. Na ni katika hikima yake kufanya ndani yake mna Aya zilizo wazi, maana yake na makusudio yake yanajuulikana wepesi. Hizi ndio msingi, ndio asli. Marejeo yote yawe juu ya hizi. Na zipo Aya nyengine za mifano, za mshabaha, zenye kutatanisha. Wengi hawawezi kuzielewa. Na wale ambao hawakubobea, hawakuzama katika ilimu, huwababaisha. Na zimeteremka hizi Aya za mifano ili wanazuoni wachungue kutafuta ilimu ndani yake, na wazingatie, na wazidi kufikiri katika jitihadi, na kufanya uchunguzi katika Dini. Lakini mtindo wa walio iacha Haki ni kutaka kuzifuata hizo Aya za mifano ili kutaka kuchochea fitna, na huzifasiri kwa kufuata matamanio yao. Na hapana anaye jua maana ya Aya hizi kwa hakika ila Mwenyezi Mungu, na wale walio thibiti kweli katika ilimu. Na hao walio thibiti husema: -Sisi tuna yakini kuwa hayo yanatokana na Mwenyezi Mungu. Sisi hatufarikishi katika kuiamini Qurani baina ya sehemu zilizo wazi (Muhkam) na zile za mifano (Mutashaabih). Na hawazingatii ila watu wenye akili iliyo nzima, ambayo haifuati pumbao na matamanio.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo
- (Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.
- Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?
- Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu
- Na kwa asubuhi inapo pambazuka!
- (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
- Basi naapa kwa mnavyo viona,
- Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia
- Hata baba zetu wa zamani?
- MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers