Surah Al Imran aya 75 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴾
[ آل عمران: 75]
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And among the People of the Scripture is he who, if you entrust him with a great amount [of wealth], he will return it to you. And among them is he who, if you entrust him with a [single] silver coin, he will not return it to you unless you are constantly standing over him [demanding it]. That is because they say, "There is no blame upon us concerning the unlearned." And they speak untruth about Allah while they know [it].
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.
Huo ndio mwendo wao Watu wa Biblia katika itikadi, ama mwendo wao katika mambo ya mali utaona: Kati yao kuna ambaye ukimpa amana ya chungu ya dhahabu au fedha atakurejeshea sawa sawa bila ya kupunguka chochote. Na mwengine kati yao ukimpa amana ya dinari moja tu hakurudushii, ila ikiwa utamshikilia mpaka aitoe. Haya ni kwa sababu wapo baadhi yao wanawaona watu wa mataifa mengine, si watu wa Biblia basi haiwalazimu wao kuwatendea haki, na wanadai kuwa hiyo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu. Na wao wanajua vyema kuwa hayo ni kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu. (Tazama katika Agano la Kale: Kumbukumbu la Torati, 23.19-20 inaruhusu kumnyonya riba mtu mbali asiyekuwa Yahudi. Kumbukumbu 12.21 inaruhusu kumlisha nyamafu mgeni na kumuuzia pia. Uzushi kama huu unakashifiwa na Aya 78 ifuatayo kuwa haya hayakutokana na Mwenyezi Mungu, bali wamepachika wao tu katika vitabu vyao.)
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi
- Enyi mlio amini! Mkiwat'ii baadhi ya walio pewa Kitabu watakurudisheni kuwa makafiri baada ya Imani
- Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni
- Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri.
- Siku itapo wafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema:
- Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu
- Na shari ya alivyo viumba,
- Akasema: Hakitakufikilieni chakula mtakacho pewa ila nitakwambieni hakika yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale
- Wala zisikushitue mali zao na watoto wao. Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwa hayo katika dunia;
- Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



