Surah Hud aya 81 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ﴾
[ هود: 81]
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut'! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Na wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipo kuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakao wafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu?
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
The angels said, "O Lot, indeed we are messengers of your Lord; [therefore], they will never reach you. So set out with your family during a portion of the night and let not any among you look back - except your wife; indeed, she will be struck by that which strikes them. Indeed, their appointment is [for] the morning. Is not the morning near?"
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Na wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipo kuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakao wafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu?
Malaika wale wakamwambia, na wao ukweli wao ulikwisha dhihiri: Ewe Lut! Usikhofu wala usihuzunike! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi, wala si binaadamu kama tuonekanavyo kwako na kwa hawa kaumu yako. Wala wao hawa hawatakufikishia shari yoyote ya kukuudhi au kukudhuru. Basi toka wewe na ahali zako usiku ukisha zagaa. Mtoke mji huu, wala yeyote katika nyinyi asigeuke kutazama nyuma, asije akaona vitisho vya adhabu naye akasibiwa na shari yake! Lakini mkeo ambaye amekukhuni, yeye hatokuwa pamoja na watao toka nawe. Yeye lazima yampate yatao wapata hawa watu. Na miadi ya kuangamia kwao ni asubuhi, na miadi hiyo ni karibu. Basi usitie khofu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi kuleni katika vile alivyo kupeni Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema
- Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika
- Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...
- Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na
- Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo
- Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
- Watakao geuka baada ya haya basi hao ndio wapotovu.
- Watayapata humo wayatakayo daima dawamu. Hii ni ahadi juu ya Mola wako Mlezi, inayo ombwa.
- Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi
- Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers