Surah Maidah aya 110 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴾
[ المائدة: 110]
Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[The Day] when Allah will say, "O Jesus, Son of Mary, remember My favor upon you and upon your mother when I supported you with the Pure Spirit and you spoke to the people in the cradle and in maturity; and [remember] when I taught you writing and wisdom and the Torah and the Gospel; and when you designed from clay [what was] like the form of a bird with My permission, then you breathed into it, and it became a bird with My permission; and you healed the blind and the leper with My permission; and when you brought forth the dead with My permission; and when I restrained the Children of Israel from [killing] you when you came to them with clear proofs and those who disbelieved among them said, "This is not but obvious magic."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!.
Na wakati huo, Mwenyezi Mungu atamwambia Isa mwana wa Maryamu miongoni mwa Mitume: Kumbuka neema niliyo kuneemesha wewe na mama yako katika dunia, nilipo kutia nguvu kwa Wahyi,(Ufunuo), na nikakutamkisha nawe ni mtoto mchanga ili kumuondolea tuhuma aliyo tuhumiwa mama yako, kama nilivyo kutamkisha nawe ni mtu mzima kwa ufunuo niliyo kufunulia; na nilipo kuneemesha kwa kukufunza kuandika, na nikakuwezesha kusema na kutenda yaliyo sawa, na nikakufunza Kitabu cha Musa na Injili niliyo kuteremshia wewe, na nikakuwezesha kutenda miujiza asiyo weza mtu mwingine kuitenda, ulipo tengeneza ndege kwa udongo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ukapuliza akawa ndege aliye hai kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, si kwa uweza wako, na ukamponesha mtoto kipofu, na ukamponesha mkoma kwa idhini na uweza wa Mwenyezi Mungu, na yakawa kwa kupitia mikononi mwako makadara ya kufufuka maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na kudra yake, na pale nilipo wazuia Mayahudi wasikuuwe na kukusalibu nilipo waletea miujiza wapate kuamini, nao baadhi yao walikanya na wakadai kuwa hiyo miujiza si lolote ila ni dhaahiri uchawi tu. (Katika Injili ya Luka inasemwa -Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.- Luka 22.43. Na katika Injili ya Yohana 5.30 Yesu anakiri: -Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.-)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Tuongoe njia iliyo nyooka,
- Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa
- Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana.
- Au wanadhani wanao tenda maovu kwamba watatushinda? Hukumu mbaya hiyo wanayo hukumu.
- Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie mbali makafiri.
- Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
- Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
- Wakati nyota zitakapo futwa,
- Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale
- Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers